UN yazitaka Hezbollah na jeshi la Israel kusitisha mapigano Lebanon Kusini
Wakikabiliwa na "maendeleo ya kutisha katika majibishano ya risasi" kwenye siku za hivi karibuni katika mpaka baina ya Israel na Lebanon, kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL leo kimezitaka Hezbollah na jeshi la Israel kusitisha uhasama.