Wekeni silaha chini wakati wa mashindano ya Olimpiki: Guterres
Kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki jijini Tokyo nchini Japan tarehe 23 mwezi huu wa Julai, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka utamaduni wa kusitisha mapigano wakati wa mashindano hayo uheshimiwe duniani kote.