Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mbu aina ya anopheles waambukizao malaria wakiwa katika maabara ya taasisi ya KEMRI/CDC nje ya mji wa Kisumu nchini Kenya
Sven Torfinn/WHO 2016

Ripoti mpya ya malaria yatoa wito wa kuchukuliwa hatua mpya za mapambano

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya malaria ulimwenguni iliyotolewa hii leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, maendeleo dhidi ya malaria yanaendelea kupungua, hasa katika nchi zenye mzigo mkubwa barani Afrika. Mapengo katika upatikanaji wa zana za kuokoa maisha yanadhoofisha juhudi za ulimwengu za kukabiliana na ugonjwa huo, na janga la COVID-19 linatarajiwa kurudisha nyuma zaidi mapambano.