Msemo wa ukielimisha mwanamke umeelimisha jamii wadhihirika Congo
Ndani ya misitu minene kaskazini mwa Jamhuri ya Congo, kunapatikana kundi la wanawake waliojitolea kusaidia jamii zilizoko maeneo ya ndani zaidi kutokomeza utapiamlo.
Ndani ya misitu minene kaskazini mwa Jamhuri ya Congo, kunapatikana kundi la wanawake waliojitolea kusaidia jamii zilizoko maeneo ya ndani zaidi kutokomeza utapiamlo.
Kupoteza mtoto wakati wa ujauzito au ujauzito usio riziki bado ni jambo linaloonekana kama mwiko kulizungumzia ulimwenguni kote, mwiko unaoambatana na unyanyapaa na aibu. Wanawake wengi bado hawapati matunzo sahihi na ya heshima wanapopoteza ujauzito au kupoteza mtoto wakati wa kujifungua.
Huduma za posta duniani zikitimiza miaka 145, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imesaka maoni ya watu kuhusu huduma hizo wakati huu ambapo baadhi wanasema tayari imejichimbia kaburi ilihali wengine wakisema ndio kwanza inashamiri.
Baada ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu hatua kwa tabianchi uliotanguliwa na harakati za vijana kutaka hatua, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Antonio Guterres aliweka tafakuri yake kwenye tahariri iliyochapishwa na ubia wa vyombo vya habari 170 wenye wasomaji zaidi ya mamilioni.
Mjadala mkuu wa mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74 ukitamatishwa hii leo jiijni New York, Marekani, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Burundi Ezechiel Nibigira amehutubia jukwaa hilo akitaka ajenda ya Burundi kwenye Baraza la Usalama iondolewe kwa kuwa hali ya usalama nchini humo ni tulivu.
Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali ni miongoni mwa waliokusanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo Ijumaa Septemba 27 kushiriki mkutano maalum wa tathimini ya hatua zilizopigwa na nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) akiwemo Rais wa Ireland, Kenya na waziri mkuu wa Fiji na Norway.
Umoja wa Mataifa unasema uchumi endelevu wa dunia ule ambao unailinda dunia na kuboresha maisha ya kila mtu kila mahali ni fursa nzuri ya kuleta ajira na masoko yenye thamani ya matrilioni ya dola. Ili kutimiza hilo , jamii ya kimataifa inahitaji kuongeza kasi ya uwekezaji.
Maendeleo ya kiuchumi
Benki, kwa pamoja, zenye mali ya thamani ya dola trilioni 47, au theluthi ya sekta nzima kimataifa, jumapili zimetoa ahadi ya kuunga mkono kanuni mpya za benki zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kukuza hatua dhidi ya tabianchi na mabadiliko kutoka mifano ya ukuaji wa uchumi "wa udhurungi hadi kijani".
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat Maimunah Mohd Sharif, miji kote ulimwenguni ni ‘sababu kuu ya mabadiliko tabianchi’ ingawa pia inaweza kuwa na suluhisho la kupunguza hewa chafuzi gesi, ambazo zinasababisha joto ulimwenguni kuongezeka.
Watu bilioni 5 duniani wako hatarini kukosa huduma za afya ifikapo mwaka 2030 endapo nchi hazitochukua hatua kuziba mapengo ya upatikanaji wa huduma za afya imesema ripoti mpya iliyotolewa leo Jumapili, wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa kufanya mkutano wa kihistoria ili kuchagiza mchakato wa haraka kuhusu huduma za afya kwa wote.