Azimio la 5 la Manama lapitishwa, watu wenye ulemavu waonesha ubingwa wao kwenye ugunduzi
Azimio la 5 la Manama limepitishwa hii leo huko Manama, mji mkuu wa Bahrain na washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji kwa Wajasiriamali likiwa na wito wa pamoja na mambo mengine likisihi jamii ya kimataifa na wadau wote katika sekta ya umma na binafsi kutumia nguvu ya ujasiriamali na uwekezaji katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii kama kitovu cha kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kupatia kipaumbele makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na familia zinazohaha kutumia uwezo wa kuzalisha ili kujikimu kimaisha.