Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la Wiki - "Pete"

Wiki hii tunaangazia neno “PETE”  na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. pete lina zaidi ya maana moja, moja ikiwa ni pambo la ahadi linalovaliwa kwenye kidole, pili ni tundu kubwa kwenye sikio la mwanamke ili kutuliwa pambo la karatasi au la herini. Maana nyingine ni pambo lenyewe la karatasi linalotiwa kwenye matundu makubwa sikioni mwa mwanamke .

Neno la wiki- Elfu au Alfu?

Katika neno la wiki tunachambua maneno alfu na elfu, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Maswala ya Mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Anasema kwamba tofauti ya matamshi ya maneno haya unatokana na uzito wa ndimi na ndiposa Kenya wanatumia elfu na Tanzania ni alfu.

Neno la wiki- Falaki

Katika Neno la Wiki hii  Septemba 16 tunaangazia neno falaki na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Neno falaki lina maana zaidi ya moja , ikiwemo elimu ya nyota,pia unajimu maana ya pili ni maisha ya kubahatisha mambo yanayotokea kulingana na elimu ya nyota. Maana ya tatu ni njia ya sayari kama vile  jua au mwezi , orbit kwa kingereza na maana ya nne ni anga lote juu tunalolitambua kama mbingu.