Mafunzo ya UNIDO yameboresha bidhaa zetu sasa tunahitaji masoko ya uhakika
Huko Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunafanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024. Zaidi ya washiriki 1000 ni wajasiriamali kutoka Afrika wakisaka kujenga mitandao na ubia ili kusaka masoko ya uhakika ya bidhaa zao na hatimaye kuondokana na umaskini, moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya Viwanda, UNIDO ofisi ya ugunduzi wa teknolojia, ITPO nchini Bahrain.