Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fanya kazi kwa bidhii utafanikiwa, acha kuwinda watu wenye ulemavu wa ngozi

Fanya kazi kwa bidhii utafanikiwa, acha kuwinda watu wenye ulemavu wa ngozi

Pakua

Imani potofu kwa baadhi ya watu ya kwamba watatajirika iwapo watapeleka  viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi kwa waganga wa kienyeji imekuwa ikikatili maisha ya binadamu hao na kuwaacha wengine na madhara makubwa  ya kisaikolojia na kimwili katika maisha yao yote, wakati vitendo hivyo vikiendelea katika jamii, hususan ya waafrika waishio kusini mwa jangwa la sahara.

Umoja wa Mataifa na wadau wamekuwa wakihimiza serikali, asasi za kiraia na jamiikuondokana na imani hizo potofu na kuthamini maisha ya kila mtu. 

Katika ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs,  lengo namba 6 linahimiza kupunguza matabaka katika jamii kwa kutowabagua watu kwa misingi mbalimbali ikiwemo ukabila, kijinsia, hali ya kiuchumi, ulemavu, rangi au asili zao.

Katika maadhimisho ya kimataifa siku ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, mwanamuziki Salif Keita ambaye pia ni mlemavu wa ngozi alitumbuiza katika moja ya kumbi za mikutano za Umoja wa Mataifa akichagiza upendo kwa jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Kwa kina zaidi basi ungana na  Patrick Newman upate burudani na ujumbe kutoka kwa gwiji huyo wa muziki kutoka Mali barani Afrika.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
4'20"
Photo Credit
Photo: UNICEF Mozambique/Sergio Fernandez