Vijana wanaokabiliana na tatizo la ajira kujihusisha na miradi ya uvuvi Burundi
Huko Burundi, Kundi la vijana limeanzisha maradi wa kujikomboa kutoka katika hali ya umasikini kwa kuanzisha kazi ya uvuvi bwawani.
Vijana hao saba wa mkoani Bubanza kaskazini magharibi mwa Burundi walianza na mabwawa madogo madogo ya uvuvi , lakini kwa sasa wamefikia viwango vikubwa vya uzalishaji wa samaki8. Pesa inayotokana na mradi huo imekuwa inasaidia kuwasomesha vijana hao katika vyuo vikuuu.