Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Hatimiliki huwezesha ubunifu kunufaisha jamii-WIPO

Aprili 26 ni siku ya hatimiliki duniani ambako katika kuadhimisha siku hii Mkurugenzi mkuu wa  shirika la kimataifa la hatimiliki, WIPO, Francis Gurry amesema, hatimiliki ni sehemu muhimu ya sekta ya ubunifu na ina faida kwa wale wanaochukua fursa ya kuzindua bidhaa mpya na huduma katika uchumi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ubunifu- kuimarisha maisha” ambako Bwana Gurry amesema licha ya kwamba ubunifu unaimarisha maisha yetu, mara nyingi jamii haichukui muda kutafakari jinsi ubunifu ulivyobadilisha kiwango cha maisha.

Nuru kwa watu asilia Afrika imeanza kung’aa: Dk Laltaika

Miaka 10 ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu hakiza jamii za watu wa asili zimeionyesha mafanikii makubwa ikiwamo nchi za Afrika kuridhia tamko hilio na hata kuanza kutumika katika ngazi ya mahakama, amesema Dk Elifuraha Laltaika, mtaalamu huru wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu jamii hizo.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa kandoni mwa mkutano wa 16 wa jamii asilia mjini New York Marekani, Dk Elifuraha amesema kuna changamoto kadhaa lakini mwanga unaonekana katika bara hilo.

Kwanza anaanza kwa kueleza mkutano huu wa 16 una maana gani?

Nuru yaangaza kwa wakazi wa vitongoji duni Nairobi, Kenya kufuatia mradi wa reli

Sekta ya usafari ni moja ya sekta ambazo zinaathiri sana maendeleo katika jamii kwani inasaidia katika sio tu usafiri wa watu bali pia wa bidhaa.

Nchini Kenya mradi wa Benki ya dunia wa kukarabati reli kwa ushirikiano na serikali ya nchi hiyo umeleta nuru sio tu katika usafiri lakini pia kwa maisha ya watu binafsi waliokuwa wakiishi vitongoji duni ambako njia za gari moshi zinapita. Basi ungana na Joseph Msami katika makala hii.

Ugonjwa wa malaria na harakati za kuutokomeza

Malaria, ni ugonjwa ambao bado unaendelea kutishia maisha ya nusu ya watu ulimwenguni kote. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO, bara la Afrika ndio linaloongoza kwa visa vya malaria kwa asilimia 90, hususan kusini mwa jangwa la Sahara ambalo linabeba mzigo mkubwa wa ugonjwa huo.

Tarehe 25 mwezi Aprili kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya malaria, lengo ni  kutokomeza gonjwa hilo.

Vikosi vya UM Haiti vyaanza kuondoka

Kuanzishwa kwa ujumbe mpya wa kuimarisha utawala wa sheria nchini Haiti ufahamikao kwa kifupi MINUJUSTH, ni mwanzo wa ujumbe unaomaliza muda wake MINUSTAH ambao ulijikita katika ulinzi wa amani, kuondoka nchini humo.

Maandalizi ya kuondoka yameanza huku baadhi ya vikosi vikiwa vimeanza safari mapema juma hili. Joseph Msami anaeleza vyema katika makala ifuatayo.

Uhaba wa malisho kwa wafugaji Uganda ni tafrani

Nchini Uganda uhaba wa malisho uliochochewa na ukame kwa wafugaji hasa wa ngo’mbe umezusha hamasa kwa wafugaji hao ambao wengi wanataka ruksa ya kulisha mifugo yao kwenye hifadhi ya taifa na serikali kwa upande wake ikisema la hasha haiwezekani. Sasa nini hatma ? ungana na John Kibego kwa makala hii.

Wanawake wavuvi wawakilisha utambulisho wa kisiwa cha Jeju

Kisiwa cha Jeju ni kisiwa kikubwa  katika rasi ya Korea. Ni moja ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyotajwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kwa kuwa na maliasili ambazo zinavutia watalii na hasa mila na tamaduni za kikundi cha wanawake na wasichana kiitwayo "jeju haenyeo” ambao hukabiliana na bahari kuvua samaki. UNESCO tayari imeingiza mila hizi katika orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Kwa undani zaidi ungana na Selina Jerobon katika makala ifuatayo..

Simu ndio daraja kati ya waliosalia Syria na wakimbizi kwingineko

Wakati mzozo wa Syria unaendelea kushuhudiwa ukiingia mwaka wa saba, raia wanakimbilia nchi jirani kuomba hifadhi. Mara nyingi wakimbizi hao kutoka Syria wanajikuta kwenye kambi zenye mazingira ya upweke huku baadhi yao mawazo yakisalia kwa familia zilizobakia nchini Syria.

Katika makala hii na Flora Nducha tunakutana na kijana Abdalla ambaye yuko na babake kambini Za’atari nchini Jordan na anasema simu ni teknolojia muhimu kwani ni daraja kati ya familia walioko Syria na wale waliokimbilia kwingineko. Basi ungana na Flora Nducha kupata undani wa Makala hii.

Simulizi ya mama mkimbizi wa Sudan Kusini aliyeko Uganda

 

Ni simulizi yenye simanzi! Familia imetawanyika kila mtu akikimbilia asikokufahamu kunusuru uhai wake. Hiyo si sehemu tu ya madhila yanayozikumba familia nyingi nchini Sudan Kusini wakati huu ambapo machafuko zaidi yanaripotiwa.

Ungana na Amina Hassan katika makala itakayokukutanisha na mama mkimbizi wa Sudan Kusini  aliyekimbilia Uganda kusaka hifadhi.

Misaada zaidi yahitajika kunusuru njaa Nigeria

Melfu ya raia nchini Nigeria wanakabiliwa na njaa hususani katika maeneo ambayo yamedhibitiwa au kuvamiwa na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Umoja wa Mataifa na mashirika yake yanahaha kutoa usaidizi wa kibinadamu wakati huu ambapo inaelezwa fedha zaidi zinahitajika ili kukidhi wingi wa mahitaji yanaoyoongezeka kila uchao. Ungana na FloraNducha katika makala ifuatayo.