Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mpatanishi anapofungasha virago ni mashaka- Dkt. Salim

Hatma ya amani Mashariki ya Kati hususan kati ya wapalestina na waisraeli imeingia dosari baada ya Marekani kutangaza kutambua Yerusalem kama mji mkuu wa Israel. Marekani ikichukua msimamo huo nchi 128 wanachama wa  wa Umoja wa Mataifa wamepitisha azimio la kuitaka nchi hiyo ibadili uamuzi huo, uamuzi ambao unaenda mbali zaidi na kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka mji mkuu wa sasa wa Israel, Tel Aviv kwenda Jerusalem. Lakini nini maana ya hatua hizi? Flora Nducha amezungumza na Dkt.

Ufugaji nyuki sasa ni mtaji dhidi ya umaskini huko Kyela, Tanzania

Kupitia lengo namba moja la kutokomeza umasikini lililomo kwenye ajenda ya  maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa  ya mwaka 2030, serikali zinahimizwa kutafuta mbinu mbadala kuwawezesha wananchi kupitia miradi mbalimbali ili kujikwamua na umasikini ifikikapo mwaka 2030.

Tanzania ni nchini mojawapo ambako serikali imechukua jukumu la kutoa elimu ya SDGs kwa kutafsiri malengo yao endelevu kwa lugha ya kiswahili ili kutoa mwongozo kwa wananchi na pili kuwapatia fursa za ujasiriamali kupitia miradi  mbalimbali kama  ufugaji, uvuvi, kilimo na kadhalika.

Vijana Somalia badilisheni simulizi potofu kuhusu vijana

Nchini Somalia wiki hii wamezindua sera ya taifa ya vijana ambayo kwayo inazungumzia hatua za kukwamua vijana kuelekea utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa mkutano wa taifa wa vijana kwenye mji mkuu Mogadishu ukihudhuria na viongozi wa kitaifa na kimataifa. Miongoni mwao ni mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana Bi. Jayathma Wickramanayake  ambaye amewasihi vijana sasa kushika usukani ili kubadili simulizi potofu ya kwamba kijana ni lazima atatumbukia kwenye misimamo mikali na kuleta ghasia.

(Picha:UN/Aliza Eliazarov)

Tumesikitishwa na kushtushwa na shambulio dhidhi ya walinda amani wetu:Mahiga

Tumeshtushwa sana na kusikitishwa na shambulio la jana dhidi ya walinda amani wetu. Amesema hayo waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga alipozungumza leo na Flora Nducha wa idhaa hii kufuatia kuuawa kwa walinda amani wa Tanzania 14, wengine 38 kujeruhiwa wakiwemo walio hali mahtuti na wanne kutojulikana walipo huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, baada ya kundi la waasi wa ADF kuzamia kituo cha walinda amani hao.

(MAHOJIANO KATI YA FLORA NDUCHA NA BALOZI AUGUSTINE MAHIGA)