Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2014

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2014

Pakua

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

Kila mwaka, Umoja wa Mataifa hutafuta vijana waliobobea katika fani mbali mbali, ambao wapo tayari kuanza huduma ya kitaaluma kama wahudumu wa kimataifa wa umma. Mpango wa Vijana Waliobobea Kitaaluma, yaani YPP, huleta vipaji vipya kwa Umoja wa Mataifa kupitia kwa mtihani wa kila mwaka.

Mwaka huu wa 2014, mtihani utafanyika mnamo tarehe 4 Disemba katika fani za Masuala ya Uchumi, Haki za Binadamu, Teknologia na Mifumo ya Habari, Upigaji Picha, Masuala ya Kisiasa, na watayarishaji wa vipindi vya Redio katika lugha za Kiarabu, Kiswahili, Kichina, na Kihispania. Kukupasha zaidi kuhusu mtihani huu, ni mwenzetu hapa Priscilla Lecomte, ambaye alijiunga na Umoja wa Mataifa kupitia programu hii ya YPP.

 

 Priscilla: Ili kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2014, uwe na shahada ya digrii, uwe unaongea Kiingereza au Kifaransa sanifu, na uwe na umri wa miaka 32 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Utatakiwa kufanya ombi la kushiriki mtihani huu kabla ya tarehe zifuatazo

 

Juni 14 hadi Agosti 13: Teknolojia na Mifumo ya Habari na Masuala ya Kisiasa

 

Juni 21 hadi Agosti 20: Masuala ya Uchumi na Utayarishaji wa Vipindi vya Redio

.

Juni 27 hadi Agosti 26: Haki za Binadamu na Upigaji Picha

 

Kumbuka, itakuwa vyema ikiwa utakamilisha na kuwasilisha maelezo yote kwa njia sahihi na nadhifu kwani hicho kitakuwa kigezo cha kupima uwezo wa wako kuufanya mtihani.

 

Kumbuka pia kuwa, maombi ambayo hayatakamilishwa vyema au yatakayochelewa kuwasilishwa hayatakubaliwa, kwa hiyo ni lazima uwasilishe ombi lako kabla ya tarehe ya ukomo.

 

Kuona kama nchi yako inashiriki,  na maelezo zaidi, tembelea tovuti:

https://careers.un.org

Photo Credit
Nembo ya UM