Operesheni za Kenya na serikali ya mpito dhidi ya Al-Shabaab zikikamilika mambo yatakuwa shwari:Mahiga
Mwakilishi maalmu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema ana matumaini operesheni za pamoja za kijeshi za serikali ya mpito na Kenya dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab zikikamilika hali ya amani itakuwa shwari Somalia.