UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya
Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.
Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu.