Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN-Habitat

Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. 

Anasema anaitwa Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei.  

Sauti
1'26"
UN News

Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya

Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.

Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.

Sauti
1'24"
UN Nairobi

Guterres: Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. 

Katibu Mkuu Guterres [GUTERESH] amesema dunia inakabiliwa na majanga lukuki, lakini Afrika ndio inaathiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa.

Sauti
9'43"
IOM

Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa takwimu hizo likinukuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, huku ikisema kuwa idadi inazidi kuongezeka kila uchao.

Sauti
1'54"