Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM

Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao. 

Waswahili husema “Mkataa kwao mtumwa” na hili ndio hasa alilowaza Bi. Lydia John Wol Mabior ambaye alikuwa ukimbizini nchini Sudan lakini huko nako vita ilipoanza akakumbuka usemi “Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani” kwani ilikuwa si hali. Anasema, “Nilipokuwa Khartoum sikulala usiku wala mchana, niliona ni bora nije kuteseka Sudan Kusini. Na leo nina furaha sana kwasababu nimefika nchini kwangu”

Lidya ya familia yake miaka kadhaa iliyopita aliikimbia nchini yake ya Sudan Kusini pale vita vilipozuka. Na shukran ziliendee shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo limefanikisha kumrejesha nchini mwake.

“Niliambiwa kuna shirikia lakutusaidia kufika Sudan Kusini, na tangu tumefika hapa eneo la Renk, tumepewa msaada wa kifedha tunamshukuru Mungu. Baada ya kusafiri kwa boti kutokea Malakal tulipewa msaada na IOM na sasa tunachotaka ni kusaidiwa Kwenda nyumbani kwetu huko Wau kwa msaada wa IOM.”

Lydia ametoa shukran zake za dhati kwa shirika la IOM na wadau wake kwa msaada wote waliowapatia katika kusaidia kuwaunganisha tena na familia zao.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
1'32"
Photo Credit
© WFP/Eulalia Berlanga