Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Utekelezaji wa ibara 13 Kenya ni mzuri licha ya changamoto

Ibara ya 13 ya tamko la haki za binadamula Umoja wa Mataifa ambalo linatimiza miaka sabini mwaka huu inasema, kila mtu ana haki ya uhuru wa kutembea na kuishi ndani ya mipaka ya nchi yake - Na kila mtu ana haki ya kuondoka na kurudi nchini mwake. 

Nchini Kenya haki hii ipo kwenye katiba ambapo Robi Chacha, Afisa kampeni usalama na haki za bindamu katika shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International, nchini humo anasema utekelezaji wake unaridhisha.

Sauti
3'37"

16 Novemba 2018

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anaangazia 

-Utapiamlo uliokithiri katika ukanda wa Sahel, ambako watoto zaidi ya milioni 1.3 wahitaji tiba haraka

-Stahamala sio tu kuvumiliana bali ni kuwa tayari kuwakubali wengine kwa misingi ya haki

-Wanafunzi na waalimu Gaza wanakabiliwa na kibarua kigumu katika shule zinazolindwa na vikosi vya Israel

-Makala leo inaangazia Ibara ya 12 ya tamko la haki za binadamu inasemaje? tega sikio

-Katika kujifunza kiswahili wajua maana ya methali "Mtondoo haufi maji"?

Sauti
10'31"
UN Photo/Martine Perret

Plastiki toka jalalani hadi ala za muziki


Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP linasema kila mbinu ni lazima itumike ili kupambana na plastiki ambazo athari zake ni kubwa sio tu kwa mazingira bali kwa mukstakabali wa binadamu na viumbe wengine baharini na nchi kavu. Na kwa mantiki hiyo limekuwa likichagiza juhudi mbalimbalimbali na ubunifu wa kugeuza taka hizo za plastiki kuwa faida katika jamii  jambo ambalo limeanza limeitikiwa na mwanaharakati wa mazingira Shady Rabab kutoka Missri. Assumpta Massoi na tarifa kamili

 

Sauti
2'
MINUSMA Video Screenshot

Sasa mke wangu hana shida ya kitu cha kupika asubuhi- Mfugaji aliyenufaika na mradi wa maziwa Gao

Nchini Mali, mradi wa kiwanda cha maziwa uliofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA umesaidia wafugaji na wazalishaji wa maziwa kuinua siyo tu vipato vyao bali pia kuimarisha uhusiano na utangamano baina yao. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

Ni katika eneo la Ansongo, lililopo kilometa 90 kutoka mji mkuu wa jimbo la Gao, Gao, ambako wakazi wake licha ya kwamba ni wafugaji na wanalizalisha kiasi kikubwa cha maziwa bado wana tatizo la kipato. Abramane Ibrahim Toure, mkazi wa eneo hili anafafanua..

Sauti
1'39"
UNRWA/Khalil Adwan

UN yahaha machafuko yanaendelea Gaza

Wakati machafuko yakiendelea kushika kasi upya kwenye Ukanda wa Gaza , Umoja wa Mataifa unasema unafuatilia haki kwa karibu huku mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo Nickolay Mladenov akishirikiana na pande zote kujaribu kurejesha utulivu.

Sauti
7'32"