Kilele cha haki za binadamu na uchambuzi wa ibara ya 30!
Leo ni siku ya haki za binadamu duniani ambapo ni kumbukizi ya miaka 70 tangu kupitishwa kwa tamko hilo tarehe 10 mwezi desemba mwaka 1948 huko Paris Ufaransa.
Miaka 70 iliyopita tamko la haki za binadamu lilipitishwa, ikiwa ni baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema kuwa kwa miaka 70, tamko la kimataifa la Haki za Binadamu limekuwa ni mhimili wa kuangaza masuala ya utu, usawa na ustawi na kuleta mwangaza wa matumaini mahala penye giza.