Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi nchini Kenya waua ndege wawili kwa jiwe moja

Mradi nchini Kenya waua ndege wawili kwa jiwe moja

Pakua

Wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea na maandalizi ya mkutano wa viongozi kuhusu mabadiliko ya tabianchi, tathmini iliyofanyika inaonyesha mafanikio yamepatikana katika kufikia lengo namba saba la malengo ya maendeleo ya milenia ambalo ni kuhakikisha uendelevu wa mazingira. Nchini Kenya mathalani, ufugaji wa nyuki ni njia moja badala ya kutunza mazingira na kuendeleza jamii katika sehemu zilizoathirika na ukame. Je mradi huo umeleta manufaa gani? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Photo Credit
Picha kutoka World Bank