Vimbunga, mvua na mafuriko makubwa Afrika Mashariki UN itaendelea kusaidia
Vimbunga, mvua na mafuriko makubwa Afrika Mashariki UN itaendelea kusaidia
Umoja wa Mataifa unasema utaendelea kuunga mkono mamlaka za Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayotokana na mvua kubwa, mafuriko makubwa na vitisho vya vimbunga ambavyo vimesababisha mamia ya vifo na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao.
Ukanda huo unakabiliwa na mvua kubwa zaidi na mafuriko makubwa ambayo yameripotiwa kuua zaidi ya watu 350 tangu mwezi Machi mwaka huu.
“Mvua inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kuwasili kwa kimbunga Hidaya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeonya jana Ijumaa Mei 3.
Tanzania
Msemaji wa WMO Clare Nullis amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva hiyo jana Ijumaa kwamba kimbunga hiki cha kitropiki ni cha kwanza cha aina yake kutokea Afrika Mashariki na kitakuwa na "athari kubwa sana."
Kulingana na Nullis, hasa Tanzania itakabiliwa na madhara, kwani ardhi ina maji mengi na "inakaribia kupata mvua zaidi."
Kenya
Kenya pia iko katika hali ya tahadhari kufuatia bwawa la maji kufurika siku ya Jumatatu ya Aprili 29, na kusababisha vifo vya takriban watu 45.
Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirika kama anavyofafanua Dkt. Stephen Jackson Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini Kenya.