Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madini kama shaba, lithium, nikeli na kobati ni muhimu kwa nishati safi: Guterres

Boti ikipita mbele ya mradi wa umeme wa upepo kutoka pwani karibu na Jiji la Yancheng mashariki mwa Uchina.
© Ruichen Hu
Boti ikipita mbele ya mradi wa umeme wa upepo kutoka pwani karibu na Jiji la Yancheng mashariki mwa Uchina.

Madini kama shaba, lithium, nikeli na kobati ni muhimu kwa nishati safi: Guterres

Tabianchi na mazingira

Madini muhimu kama vile shaba, lithiamu, nikeli, kobati na madini adimu hapa duniani ambayo ni sehemu muhimu kwa ajili ya teknolojia ya nishati safi, ikijumuisha mitambo ya upepo, paneli za sola, magari ya umeme na uhifadhi wa betri amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Akizindua jopo maalum mjini New York Marekani kwa ajili ya mchakato wa kuhamia nishati shafi Antonio Guterres amesema “Kuongezeka kwa mahitaji ya madini haya ili kuchochea mapinduzi ya nishati kunaleta hatari, changamoto na fursa, haswa kwa nchi zinazoendelea. “

Ili kukabiliana na hali hiyo, Katibu Mkuu anatumia nguvu ya Umoja wa Mataifa ya kuitisha kukusanya kundi la watu tofauti na uwakilishi la serikali na watendaji wasio wa serikali ili kuwezesha kuwezesha kuwepo na viwango na ulinzi, na kujumuisha haki, katika mchakato huu wa mpito kuelekea nishati mbadala.

Jopo hilo jipya lililoanzishwa kuhusu madini muhimu lna mchakato wa  mpito wa nishati likiongozwa na Balozi Nozipho Joyce Mxakato-Diseko wa Afrika Kusini na Bi. Ditte Juul Jørgensen mkurugenzi mkuu wa nishati kutoka Tume ya Muungano wa Ulaya litaundakanuni za kimataifa za pamoja na za hiari kuongoza serikali na wadau wengine wanaohusika katika minyororo muhimu ya thamani ya madini katika miaka ijayo kwa kushughulikia masuala yanayohusu usawa, uwazi, uwekezaji, uendelevu na haki za binadamu.

Haki ni kitovu na mkakati huo

Kwa mujibu wa Guterres kanuni moja inayong'aa kutoka na kiini cha mkakati huu ni haki.

Amesema haki kwa jamii ambako madini muhimu yanapatikana na nimemaliza kusoma kitabu Cobalt. Na kwa hivyo ninafahamu haswa jinsi jamii zinavyoteseka katika hali hizi.

Ameendelea kuongeza kuwa haki kwa nchi zinazoendelea katika uzalishaji na biashara na haki katika mapinduzi ya nishati duniani.

Na ameweka bayana kwamba Mapinduzi hayo sasa yamepamba moto.

Nishati mpya ya upepo iliongezeka kwa asilimia 60  mwaka jana, ikilinganishwa na 2022 na nishati ya mpya ya jua ilipaa kwa asilimia 85 kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati IAEA.

Kwa hivyo amesema “hakuna swali, taa zinazimika wakati wa enzi ya mafuta na hii bila shaka ni muhimu ikiwa tunataka kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na ikiwa tunataka kuhakikisha joto haliongezeki zaidi ya nyuzi joto kuweka 1.5 na hili bado linawezekana“.

Amesisitiza kuwa hivi “Sasa, mbinu za kuchelewesha kutoka kwenye tasnia ya mafuta kisukuku haziwezi kubadilisha hilo. Taarifa potofu, upotoshaji na kuzunguka haviwezi kubadilisha hilo haijalishi ni mabilioni mangapi ya dola hutupwa huko.”

 Lazima tuhamie Kwenye nishati safi na kutokomeza mafuta kisukuku

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa Lakini ili kuzuia machafuko makubwa zaidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5 ni lazima tuongezei zaidi usambazaji wa nishati mbadala, na kukomesha matumizi ya nishati ya mafuta  kisukuku.

Tunahitaji kupindua ukurasa

Guterres ameongeza kuwa kati ya sasa na mwisho wa muongo huu sehemu ya umeme inayozalishwa na nishati ya mafuta lazima ipungue kutoka asilimia 60 hadi 30. 

Na mgao unaotokana na vifaa vinavyoweza kurejelezwa lazima kupanda kutoka asilimia 30 hadi 60 kulingana na IAEA na madini muhimu ndio msingi wa mabadiliko haya.

Amesema Dunia inayowezeshwa na nishati mbadala ni Dunia iyenye njaa ya shaba, lithium, nikeli, kobati na madini menine nadra ya Dunia.

Ametolea mfano magari ya umeme akisema yanahitaji mara sita zaidi ya madini haya kuliko magari yanayotumia nishati ya mafuta. Mashamba ya nishati ya upepo wa pwani yanahitaji mara kumi na tatu zaidi ya mitambo sawa ya gesi. Katika dunia inayoelekea kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050, Shirika la IAEA linakadiria mahitaji ya madini muhimu kuongezeka mara tatu na nusu katika muongo huu.

Pia amesema sasa “kwa nchi zinazoendelea zenye hifadhi kubwa, madini muhimu yanawakilisha wazi fursa muhimu, fursa ya kuunda ajira, kuwa na uchumi mbalimbali, na kuongeza kipato. Lakini pia zinaweza kuwa chombo muhimu ili kuhakikisha kwamba nchi hizi zinaweza kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Kwa urahisi, ni muhimu kwamba kila kitu kidhibitiwe vyema”.

Amesema nchi nyingi zinazoendelea hazijafaida kwa kuwa na madini hayo na hilo ni lazima libadilike.

Kwa hivyo amesema nchi zinazoendelea haziwezi kuachwa nyuma na mnyororo wa thamani ya nishati safi inayoachiliwa kwa wasambazaji wa malighafi za Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema ni muhimu kabisa kwamba thamani iliyoongezwa ifanyike katika nchi zinazozalisha malighafi hizi na kwamba thamani iliyoongezwa haiko katika nchi zilizoendelea pekee. Kwa sababu hapo ndipo sehemu kubwa ya mnyororo wa thamani hufanyika.

Kuhusu jopo 

Amesema jopo hilo litasaidiwa na sekretarieti ya kiufundi kutoka kwa Timu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa mataifa UNEP, tume ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD na taasisi kadhaa za mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Kwa hivyo amesema jopo hilo ni sehemu muhimu ya hatua za Umoja wa Mataifa.

Amesema nyinyi wajumbe wetu wa jopo kutoka kwenye serikali, sekta, mashirika ya kiraia na zaidi ni ushahidi kwamba kuna nia ya kweli ya kufanya mambo kwa njia tofauti. Kila sauti lazima isikike. Na ninakaribisha sana ushiriki wako.”

Tunachotafuta amesema ni haki, uwazi, uwekezaji, uendelevu na haki za binadamu. Na wanapaswa kuchota kutoka kwa viwango na mipango iliyopo kuviimarisha. Na bila shaka mapengo mengi bado yanahitaji kuzibwa.