Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watu wa jamii za asili Kenya

Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).
UN News/Assumpta Massoi
Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).

Jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watu wa jamii za asili Kenya

Tabianchi na mazingira

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki wa jukwaa hilo na mmoja wao ni Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza jinsi mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.