Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Watoto wenye mahitaji maalum wabadilisha maisha yao: OCHA

Noureldin akiwa na mama yake na ndugu yake.
© Save the Children/Khalid Abdulfattah
Noureldin akiwa na mama yake na ndugu yake.

Sudan Watoto wenye mahitaji maalum wabadilisha maisha yao: OCHA

Wahamiaji na Wakimbizi

Noureldin Abdelwahid mwenye umri wa miaka 12, anaishi na wazazi wake na ndugu zake 11 kwenye makazi yenye mkusanyiko wa wakimbizi wa ndani (IDPs) huko Ed Damazine, mji mkuu wa Jimbo la Blue Nile, kusini-mashariki mwa Sudan. Noureldin alipata polio alipokuwa mdogo, ambayo iliathiri maisha yake sana.

Baba yake, Elnour, anaeleza kuwa "hatukujua mengi kuhusu hali yake, na pia tulikuwa tunahaha kujikimu tkiuchumi, kwa hiyo hatukuzingatia sana, kwa bahati mbaya, na kwa sababu hiyo, Noureldin anaishi na ulemavu wa kimwili."

Noureldin hawezi kutembea na anaweza kutumia mkono mmoja tu anakumbuka "nilipokuwa mdogo, mama yangu alikuwa akinisaidia. Alikuwa akinileta bafuni, na kunioogesha na kunibeba. Lakini sasa nimekuwa mtu mzima hawezi kufanya hivyo tena. "

Kama vile wakimbizi ndani wengine wengi walio katika mazingira magumu nchini Sudan, Elnour anajitahidi kuhudumia familia yake na kukidhi mahitaji yao ya msingi, yeye ni mtu anayelipwa mshahara wa kila siku, ambayo ilifanya iwe karibu kutowezekana kwake kumnunulia Noureldin kiti mwendo, haswa baada ya vita kuzuka kati ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan na Vikosi vya msaada wa Haraka (RSF), katika mji mkuu, Khartoum, Aprili 2023.

Noureldin anasema “Nisingeweza kuondoka nyumbani ilikuwa vigumu sana kutambaa kwenye udongo wenye mawe na matope, na ningependelea kukaa nyumbani,siku moja nilianguka na kuumiza sikio langu na upande wa kushoto wa uso wangu,” aliongeza huku akionyesha kovu usoni na kichwani.

Noureldin akiwa katika sehemu salama kwa watoto.
© Save the Children/Khalid Abdulfattah
Noureldin akiwa katika sehemu salama kwa watoto.

Kwa bahati nzuri, maisha ya Noureldin yalibadilika wakati familia yake ilipoanza kupokea usaidizi kupitia uingiliaji kati uliofadhiliwa na SHF, ilianza kwa kutembelewa na mjumbe wa Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto wa Kijamii, uliofunzwa na Save the Children.

Elnour alieleza: "Sheikh [kiongozi wa jadi] ambaye anaongoza mtandao alikuja nyumbani kwetu na kuuliza kuhusu kesi ya Noureldin."

Kufuatia ziara hiyo, familia ilipokea chakula na vifaa visivyo vya chakula, na Noureldin akapokea kiti cha magurudumu, kilichobadilisha maisha yake na uhamaji wake.

"ilibadilisha kila kitu kwangu na kwa familia yangu, sasa naweza kwenda nje na kufurahia wakati na marafiki zangu," alisema, akiongeza kwamba huenda kwenye nafasi ya kirafiki ya watoto inayoungwa mkono na Save the Children karibu na kucheza na wenzake.

Kwa bahati nzuri, maisha ya Noureldin yalibadilika wakati familia yake ilipoanza kupokea msaada kupitia uingiliaji kati uliofadhiliwa na SHF, ilianza kwa kutembelewa na mjumbe wa Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto wa Kijamii, uliopewa mafunzo na shirika la Save the Children.

Noureldin akiwa na wafanyakazi wa Save the Children katika sehemu salama kwa watoto.
© Save the Children/Khalid Abdulfattah
Noureldin akiwa na wafanyakazi wa Save the Children katika sehemu salama kwa watoto.

Msaada kwa Noureldin

Elnour anasema "Sheikh ambaye anaongoza mtandao huo alikuja nyumbani kwetu na kuuliza kuhusu kesi ya Noureldin."

Kufuatia ziara hiyo, familia ilipokea msaada wa chakula na vifaa visivyo chakula, na Noureldin akapokea kiti mwendo, kilichobadilisha maisha yake na uhamaji wake.

"Msaada huo ulibadilisha kila kitu kwangu na kwa familia yangu, sasa naweza kwenda nje na kufurahia pamoja na marafiki zangu."

Anaendelea kusema kwamba "Ninakuja hapa na kaka zangu, na tunacheza na watoto wengine, ni vizuri." 

Wakati yeye na kaka zake wana shughuli nyingi za kucheza na marafiki, wazazi wao wana wakati mwingi wa kwenda sokoni na kufanya kazi, "baba yangu sasa anaweza kutununulia tende, unga na mafuta," ameongeza.

Mradi huo unaofadhiliwa na SHF na kutekelezwa na Shirika la Save the Children, unalenga kusaidia watu wapatao 30,500 wakiwemo watoto na watu wazima wanaoishi na ulemavu kwa afua za ulinzi, maji safi, usafi wa mazingira na usafi katika Jimbo la Blue Nile, na ni sehemu ya mradi mkubwa wa kukabiliana na dharura, ambao pia hutoa huduma za afya na lishe kwa watu wanaohitaji.

Mradi huu unatekelezwa kwa pamoja na Save the Children, Child Development Fund na Alsalam Organization for Rehabilitation and Development.

Noureldin akiwa na familia yake.
© Save the Children/Khalid Abdulfattah
Noureldin akiwa na familia yake.

Kuchangia katika jamii

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada yad harira OCHA kupitia mradi huo, Elnour sasa anaweza kuchangia masuala mengi ya jamii, kama vile kuhudhuria ndoa na mazishi, ambazo ni shughuli muhimu kwa hadhi ya familia.

Mama wa Noureldin, Halima, anasema “maisha yetu yameboreka sana kwa msaada huu wa ziada, lakini muhimu zaidi ninafurahi kuona Noureldin akifurahia wakati wake sasa na marafiki zake, pia amejifunza kuandika katika mahali maalum kulikotengwa kwa ajili ya watoto na rafiki zao hatua ambayo itamruhusu kurudi kwenye masomo yake hivi karibuni."

Wakati huo huo, Elnour anatumai kuwa familia yake haitahamishwa tena "mamilioni ya watu kwa sasa wanakimbia kutoka Kwenye maeneo yenye migogoro huko Khartoum, Darfur na majimbo mengine, hadi sasa, eneo letu limekuwa salama kiasi, tunaomba kila siku iwe shwari na kwamba sehemu nyingine ya Sudan iweze kurejea katika amani.”

Takriban miezi 10 baada ya vita kuzuka, Sudan inakabiliwa na moja ya migogoro inayokua kwa kasi zaidi duniani, ikiwa na mahitaji ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika kipindi kifupi kama hicho. 

Takriban watu milioni 25, ambapo zaidi ya milioni 14 kati yao ni watoto wanahitaji msaada wa kibinadamu, na zaidi ya watu milioni 7.6 karibu asilimia 15 ya wakazi wa Sudan wamekimbia makazi yao tangu 15 Aprili. 

Kulingana na takwimu mpya kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Sudan sasa ndio mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi duniani, ukiwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani milioni 9, ikiwa ni pamoja na watu waliokimbia makazi yao kabla ya Aprili 2023.