Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya kompyuta shule ya msingi yapunguza utoro

Watoto kama hawa kutoka Sudan wakisoma kwa kutumia kompyuta.
© UNICEF/Shehzad Noorani
Watoto kama hawa kutoka Sudan wakisoma kwa kutumia kompyuta.

Matumizi ya kompyuta shule ya msingi yapunguza utoro

Utamaduni na Elimu

Matumizi ya tehama katika kufundishia wanafunzi wa shule ya msingi nchini Kenya yaliyofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF yameongeza ufaulu wa watoto na kupunguza utoro.

Huyo ni James Lokeny, mwanafunzi ya darasa la 8 katika shule ya msingi ya Namoruputh iliyoko kaunti ya Nakuru nchini Kenya akieleza kuwa hapo awali kabla ya UNICEF kuwafungia intaneti katika shule yao mawasiliano yalikuwa mabovu lakini sasa ni mazuri na wanaweza kusoma kwakupitia kompyuta ndogo au tablet.

Anasema akijifunza kupitia kompyuta masomo yanakuwa rahisi kwakuwa ana uwezo wa kuona vitu vingi ikilinganishwa na kujifunza darasani pekee kwakutumia kitabu na anafuraha maana tayari matokeo yake yanaonesha ufaulu umeongezeka.

Mwalimu Justus Kingoo anasema zaidi ya kufaulu sasa hakuna utoro kwa wanafunzi .

"Sasa, wengi wao kwa kuwa wanaweza wakajifunza wenyewe, na wakagundua vitu wenyewe, mtazamo wao umebadilika sana. Wakiwa na hizi komptuta ndogo kujifunza kwao kunavutia, kwasababu kuna njia mbalimbali za kuipata taarifa moja. Unapata kuona hamu ya wanafunzi wengi. Mathalani, ukiwaambia kesho somo hili tutasoma kidijitali, hakuna hata mtu mmoja atakaye kosa shule."

Naye Andrew Brown, mkuu wa mawasiliano,uhamasishaji na uhusiano wa UNICEF  nchini Kenya anaeleza sababu za kuwekeza kwa wanafunzi hawa wa vijijini .

“Duniani kote, kupitia program yetu ya kujifunza ya kufikiria upya, tunajaribu kufanya kusoma kwa kupitia mtandao kuwa miongoni mwa haki zao za msingi za kusoma kama masomo mengine, kwa wanafunzi wote. Na hii itasaidia kuondoa utofauti mkubwa uliopo baina ya wanafunzi ambao wanauwezo wa kupata masomo kijiditali, na wale ambao hawana uwezo huo. Na utofauti huu mkubwa, ulionekana zaidi wakati wa janga la coronavirus">COVID-19 ambapo wanafunzi wenye uwezo wa kupata mitandao walikuwa wakiendelea na masomo, wakati wale wengine wakishindwa kuendelea na masomo.”

Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanahamasisha kuondoa utofauti baina ya  matabaka katika jamii, kuleta usawa pamoja na kuhakikisha watu wote wanapata elimu bila kumuacha mtu yeyote nyuma.