Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante UNAMID kazi mmeitimiza:UN/AU

Shule ya Oumoul Mouminina katika eneo la  Forobaranga Darfur Magharibi ikilindwa na UNAMID
UNAMID/Albert González Farran
Shule ya Oumoul Mouminina katika eneo la Forobaranga Darfur Magharibi ikilindwa na UNAMID

Asante UNAMID kazi mmeitimiza:UN/AU

Amani na Usalama

Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika AU, Moussa Faki Mahamat na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakizungumzia maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Muungano wa Afrika la amani na usalama na Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa, leo ndio siku ya mwisho ya mpango wa pamoja wa vyombo hivyo viwili wa kulinda amani Darfur Sudan ujulikanao kama UNAMID.

Maamuzi ya Baraza la amani na usalama la AU yalipitishwa tarehe 30 Novemba 2020 na ya azimio namba 2559 (2020) la Baraza Kuu la tarehe 22 Desemba 2020

yaliafiki kuuvunja mpango wa UNAMID ifikapo 31 Desemba 2020.

Viongozi hao Bwana Msahamat na Guterres wamesema kuanzishwa kwa mpango huo wa aina yake miaka takriban 13 iliyopita ilikuwa ni hatua ya kihistoria ambapo mashirika yote mawili AU na UN, nchi zilizochangia wanajeshi na polisi na wahisani wameshiriki katika juhudi za pamoja za kuwalinda rai ana kusaidia ujenzi wa amani Darfur.

Kikosi cha askari wa UNAMID kutoka China kikiwa Nyala Februari 2010
UNAMID/Albert González Farran
Kikosi cha askari wa UNAMID kutoka China kikiwa Nyala Februari 2010

Mwenyekiti wa Au na Katibu Mkuu kwa pamoja wameishukuru UNAMID kwa kazi kubwa na kurejea ahadi yao ya kuendelea kuisadia serikali na watu wa Sudan katika kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika mchakato wa amani na utekelezaji wa mpango wa kitaifa wah atua katika kuwalinda raia.

Pia wametoa wito kwa wadau wote wa Sudan kuhakikisha usalama na mpangilio wa kuondoka kwa mpango wa UNAMID katika kipindi cha miezi sita ijayo na kuruhusu mpango mpya wa usaidizi utakaochukua nafasi ya UNAMID ujulikanao kama UNITAMS.