Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani shughulikia ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine wa makusudi: Wataalam

Huko Brooklyn, New York, waandamanaji waandamana  kwa amani dhidi ya dhuluma za polisi.
UN News/Daniel Dickinson
Huko Brooklyn, New York, waandamanaji waandamana kwa amani dhidi ya dhuluma za polisi.

Marekani shughulikia ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine wa makusudi: Wataalam

Haki za binadamu

Takribani  wataalam huru 30 walioteuliwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa wameitaka Marekani ifanyie mabadiliko mfumo wake wa haki na uhalifu kufuatia mauaji ya hivi karibuni ya wamarekani weusi ikiwemo mikononi mwa polisi.

Katika taarifa yao iliyotolewa leo Ijumaa wataalam hao ameitaka mamlaka ya Marekani kushughulikia utaratibu wa ubaguzi wa rangi na upendeleo wa rangi na kufanya uchunguzi huru katika kesi za utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaofanywa na maafisa polisi.

Wataalam hao wamelaani vikali ubaguzi wa rangi wa siku hizi nchini Marekani na kutaka kuchukuliwa hatua Madhubuti kukabiliana na utaratibu uliomea mizizi wa ubaguzi, machafuko ya polisi, ukwepaji wa sheria na upendeleo katika mfumo wa haki  za wanchi, hii ni baada ya kushuhudiwa mauaji mengi ya Wamarekani weusi.

Mizizi yake katika utumwa

Mizizi ya ubabe wa polisi nchini Marekani ilianza kale na doria za utumwa na udhibiti wa kijamii ambapo watumwa walikuwa wakihodhiwa kama bidhaa wamiliki wao walitaka kulindwa kutokana na machafuko na ukwepaji sheria dhidi ya watu wenye asili ya Afrika.

Na hivyo nchini Marekani hulka hii ya ubaguzi wa rangi ni dhahiri katika vitendo vinavyofanywa na polisi zama hizi .

Wataalam ambao wanachunguza ukiukwaji wa haki za binadamu ama kuhusu nchi fulani au masuala kadhaa wamelaani mauaji ya mwezi Februari na mwezi Machi ya Ahmaud Arbery na Breonna Taylor na haya ya 25 Mei ya George Floyd ambaye kifo chake akiwa mikononi mwa polisi kimesababisha maandamano makubwa yanayoendelea nchi nzima Marekani na katika miji mbalimbali duniani.

Bwana Arbery mwenye umri wa miaka 25 aliuawa kwa kupigwa risasi na wanaume watatu wazungu wakati akifanya mazoezi ya kukimbia karibu na nyumbani kwake, huku Bi. Taylor naye mwenye miaka 25 alipigwa risasi kitandani kwake wakati polisi walipovamia kupekuwa nyumba ambayo siyo iliyokusudiwa.

Bwana Floyd aliyekuwa na umri wa miaka 46 aliuawa baada kukamatwa na polisi mjini Minneapolis kwa madai ya kutumia noto bandia.

Video ya polisi aliyemkandamiza na goti shingoni , huku wengine watatu wakishitiki na kuangalia hadi akikata roho imezusha ghadhabu kubwa kote duniani.

 

Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji kote Marekani ikiwa ni pamoja na jiji la New York kudai kuzingatiwa kwa haki za wamarekani weusi.
UN /Shirin Yaseen
Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji kote Marekani ikiwa ni pamoja na jiji la New York kudai kuzingatiwa kwa haki za wamarekani weusi.

 

Mauaji yameaamsha hisia za mauaji

Wataalam hao wamesema kwamba mauaji haya yamehusisha ukwepaji sharia, kutojali au kutothamini Maisha ya mt una matumizi ya maeneo ya umma kudhihirisha ukandamizaji wa rangi vinadhihirisha kwa kila njia mauaji ya kikatili ya zama hizi.

Video ya karibuni ikionyesha wazungu wanamkimbiza, kumbana na kumuua kijana ambaye alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia au kumuonyesha afusa wa polisi na uzito wake wote akipiga goto kwenye shingo ya mtu kwa zakika nane imeushangaza ubinadamu na kuamsha hisia za kigaidi kwamba hyo ndio yaliyokusudiwa kudhihirishwa na utawala wa mauaji nchini Marekani .”

Wameongeza kuwa ukizingatia historia ya ukwepaji sharia kwa ukatili wa ubaguzi wa rangi wa aina hii hapa Marekani , watu weusi wana kila sababu ya kuhofia maisha yao.

Wakati mamilioni ya Wamarekani wakimiminika mitaani kuandamana wataalam hao wameelezea hofu yao kuhusu hatua za polisi dhidi ya waandamanaji hao.

Wamesemamaandamano yanaambatana na machafuko, kutu kukamatwa, wanajeshi kumiminwa mitaani na maelfu ya waanfdamanaji kuswekwa rumande ambapo baadhi yao wamekabiliwa na unyanyasaji na udhalilishwaji.

Wataalam hao 28 waliotia Saini taarifa hii waliteuliwa na Baraza la haki za binadamu ama kwama wawakilishi maalum au wajumbe wa makundi mbalimbali yanayofanyakazi kwa ajili ya haki za binadamu. Sio wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na hawalipwi na Umoja wa Mataifa.