Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Familia huko Gaza zinatatizika kupata chakula cha kutosha.
© WFP/Ali Jadallah

Baada ya kulazimishwa kuondoka Rafah baadhi ya wapalestina warejea kwenye nyumba zao zilizoathiriwa na mabomu

Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.

Sauti
2'32"
Dkt. Hashim Hussein, Mtaalamu wa kuendeleza uwekezaji katika shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO akizungumza na Assumpta Massoi huko Bahrain.
UN News/Abdelmonem Makki

Harakati za uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain

Jukwaa la 5 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 linaanza kesho kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama ukileta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo wajasiriamali kutoka pembe zote za dunia. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na na maudhui ni kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuendeleza uvumbuzi na ukuaji wa kiuchumi. Jukwaa hili linalenga basi kupatia majawabu changamoto za dunia ikiwemo umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi, amani, haki kwa muktadha wa SDGs.

Sauti
4'28"