Juhudi zahitajika ili kila mtu wakiwemo wakimbizi wapate haki ya huduma za afya - WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO linafanya juhudi kubwa za kuelimisha umma kuhusu mahitaji na changamoto za afya zinazowakabili wakimbizi na watu wengine wanaolazimika kuzikimbia nyumba zao.