Bioanuwai: Ni nini, na tunawezaje kuilinda?
Umoja wa Mataifa na wadau wake ulimwenguni wanakabiliana na upotevu mkubwa wa wanyama na mimea, tarehe 23 Januari wanakutana jijini Nairobi, kenya kujadili jinsi ya kuepuka upotevu huo, katika mkutano mkuu ambao utaangazia bioanuwai ni nini, na jinsi gani Umoja wa Mataifa, unaweza kusaidia juhudi za kuwezesha asili kuishi na kustawi.