FAHAMU UMOJA WA MATAIFA
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Zaidi ya watu milioni moja kusini mwa Madagascar wanahaha kupata mlo, nah ii inaweza kuwa ni tukio la kwanza kabisa duniani la watu kukumbwa na njaa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP.
Tarehe 8 Oktoba, sauti ya makofi makubwa na yasiyo ya kawaida ilisikika karibu na chumba cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi. Vita vilivyopiganwa kwa miongo kadhaa na wanaharakati wa mazingira na watetezi wa haki, mwishowe vilizaa matunda.
Sambamba na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 74/225, Katibu Mkuu Ijumaa hii ya tarehe 24 Septemba ameandaa mjadala wa ngazi ya juu wa Nishati wakati huu wa Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 ili kuharakisha utekelezaji wa lengo namba 7 la maendeleo endelevu linalohusiana na nishati endelevu.
Azimio la Durban Iilipitishwa kwa kauli moja katika mkutano wa dunia wa mwaka 2001 dhidi ya Ubaguzi wa rangi (WCAR) uliofanyika huko Durban, Afrika Kusini.
Je unaposikia nchi zilizoendelea zinahamasishwa kutoa fedha kufanikisha miradi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi unaelewa nini?. Je ni nani anasimamia fedha hizo, zinatumika kwenye maeneo gani? nani ananufaika na fedha hizo na uamuzi wa kuanza kuchanga ulitokea wapi?
Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza tarehe 14 Septemba, na uko tofauti sana na mkutano wa mwaka jana 2020 ambao wote ulikuwa ni kwa njia ya mtandao.
Ongezeko la chuki na uhalifu dhidi ya watu wenye asili ya Asia na visiwa vya Pasifiki nchini Marekani tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19 limemhamasisha mmoja wa wasanii wa uchoraji hapa Marekani kuchora Sanaa mbalimbali zilizogonga vichwa vya Habari kote duniani
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema ukiukwaji wa haki za binadamu jimboni Tigray nchini Ethiopia umefurutu ada na sasa mapigano yanayoendelea yamesambaa katika majimbo ya Jirani ya Afar na Amhara na kutishia kusambaa katika eneo lote la pembe ya Afrika.
Wavuvi na wataalamu wa masuala ya uvivi katika ziwa Tanganyika nchini Tanzania wameelezea changamoto wanazokutana nazo zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.