Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: FAO/Danfung Dennis

Uvumbuzi wa mashine ya kukausha nafaka ni habari njema kwa mkulima Thika, Kenya

Wakulima wengi hukumbwa na changamoto za kuhifadhi mazao yao baada ya kuyavuna hususan nafaka hali inayawaletea hasara kubwa ya kupoteza chakula na hali kadhalika kusababishia familia zao taabu kama vile ukosefu wa chakula. Sasa mkulima mmoja nchini Kenya David Burii, amebuni kifaa kinachowasaidia wakulima kukausha nafaka yao kwa njia rahisi. Mwandishi wetu kutoka Kenya Jason Nyakundi alimtembelea kwenye karakana yako huko Thika na kututumia ripoti hii.

Sauti
2'53"
UN Photo/Sophia Paris

Tukiwainua walezi, tunaiinua familia nzima-Mary Mafwimbo

Na punde ni makala ambapo leo tunaelekea Tanzania kusikia harakati za msichana ambaye ameanzisha ‘shirika la kiraia la kuhudumia wanawake, wazee na watoto huko mkoani Morogoro.

Na sasa ni wakati wa makala ambapo John Kabambala wa radio washirika Kids Time FM ya Morogoro  nchini Tanzania anaangazia shughuli za shirika lisilo la kiserikali  la Morogoro  organization for women aid and child support MOWACS katika kusaidia wanawake wazee na watoto. Msichana Mary Mafwimbo aliyelianzisha shirika hilo anaanza kwa kueleza lengo lake kuu.

Sauti
3'7"
Photo: IRIN/A. Morland

Jinamizi la ndoa za mapema katika jamii ya wafugaji wa Kiturkana, Kenya

Ndoa za mapema ni jinamizi kubwa lilalowandama watoto wa kike hasa katika jamii za wafugaji duniani kote, kutokana na tabia ya kulinganisha mtoto wa kike na maelfu ya mifugo. Jamii hizo ni pamoja na Karamajong Kaskazini Mashairki mwa Uganda, Toposa wa Kusini mashariki mwa Sudani Kusini na Masai na Turkana nchini Keenya.

Katika jamii ya Turkana Kenya, ndoa hizo ni sehemu ya utamaduni wao na unaathiri vibaya ustawi wa watoto wa kike na uke wao mbeleni.

Sauti
3'43"
FAO/Alessandra Benedetti

IFAD yarejesha matumaini ya wakulima wa milimani Morocco

Nchini Morocco mradi unaofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya kilimo wa Umoja wa Mataifa, IFAD umeendelea kuwa na mafanikio makubwa hususan kwa wanufaika ambao ni wakazi wa milimani. Mradi huo ulioanza mwaka 2011 na unatamatishwa mwaka huu wa 2019  unalenga watu 33,000 wengi wao wakiwa ni wakulima na wafugaji wadogo ambao ni pamoja na wanawake, vijana na wakulima wasiomiliki ardhi. Makundi haya ni yale ambayo yanaathirika na mnyororo wa thamani wa mazao kama vile matufaha na mizeituni.

Sauti
3'
UN News/ John Kibego

Wakimbizi wakaribisha mradi wa WFP kuimarisha “lishe”, Uganda

Jamii za wakimbizi kote duniani hukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa lishe na uhakika wa chakula kutokana na ukata wa ufadhili na kutokuwa na ardhi ya kutosha ili kujishughulisha na kilimo. Hii mara nyingi husababisha watoto kudumaa na kusalia katika hatari ya kuungwa magonjwa mbalimbali.

Katika juhudi za kushughulikia chagamoto hizo, shirka la mpango wa chakula duniani (WFP), linatekeleza mradi wa ushirikiashaiji wa wakimbizi ambapo wanatumia kipande kidogo cha ardhi kupata lishe amabao umekaribishwa na wakimbizi.

Sauti
3'45"
UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi

Ubunifu wa spika janja Kaya sasa kuanza kuingia sokoni mwakani

Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuleta mabadiliko katika dunia ya sasa na kuhakikisha mustakabali wa kizazi kijacho unakuwa bora. Umoja wa Mataifa ukitoa wito huo vijana nao wanaitikia kuhakikisha kuwa wanatumia stadi zao kubadilisha maisha ya jamii zao kwa kuzingatia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa vijana hao ni Isaya Yunge kutoka Tanzania ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni inayotengeneza spika janja, Smart Kaya.

Sauti
4'26"
Photo: FAO

Tuligundua kwa kukuza uchumi wa mwanamke, tutakuza uchumi wa jamii nzima-Paul Siniga

Asasi ya African Reflections Foundation inayojishughulisha na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs nchini Tanzania, kwa miaka mingi imejikita katika kuleta usawa wa kijinsia nchini humo kwa njia ya kukuza ushiriki wa shughuli za uchumi kwa wanawake. Asasi hiyo inatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake katika shughuli za kilimo kuanzia hatua ya mwanzo hadi hatua ya masoko. Paul Siniga, Mtendaji Mkuu wa asasi hiyo akihojiwa na Idhaa ya Kiswahilli ya Umoja wa Mataifa anafafanua namna wanavyotekeleza miradi hiyo.

 

Sauti
3'15"
UNMISS/Eric Kanalstein

'Liz Mazingira' asongesha kasi ya Hayati Profesa Wangari ya upanzi wa miti nchini Kenya

Nchini Kenya, harakati za upanzi wa miti zilizochochewa na Hayati Profesa Wangari Maathai bado zinazidi kushika kasi kila uchao hasa wakati huu ambapo harakati hizo zinaongozwa na msichana Elizabeth Wanjiru Wathuti al maarufu Liz Mazingira mwenye umri wa miaka 23. Liz Mazingira ametambuliwa sana nchini Kenya na pia Kimataifa kwa juhudi zake za utunzaji wa mazingira kwa njia ya upanzi wa miti, na kwa kuhamasisha  wengine kufanya hivyo, baada ya kupanda mti wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka saba. Je sasa anafanya nini?

Sauti
4'8"
UN/maktaba

Wanafunzi wa kike huko Morogoro na ndoto zao kwa siku za usoni

Upatikanaji wa elimu kwa wote bado ni lengo ambalo halijafanikiwa kwa asilimia mia kwa mia kutokana na sababu mbali mbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa haki hiyo. Kwa upande wa mtoto wa kike, upatikanaji wa elimu unakwamishwa na mambo mbali mbali iikiwemo, ndoa za mapema, ukeketaji, mimba za utotoni na hata ukosefu wa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi lakini pale ambapo wasichana wanapata nafasi ya kuhuduria shule uwezo wao ni mkubwa vile vile ndoto zao. Hali hiyo inadhihirika katika makala ifauatayo ya John Kabambala wa radio washirika Kids Time FM ya Morogoro, ungana naye.

Sauti
3'12"
Photo: IRIN/A. Morland

Vijana Kenya wasimama kidete kunufaika na mradi wa uchimbaji mafuta Turkana

Nchini Kenya, kugundulika kwa mafuta kaskazini mwa nchi hioyo kumefungua fursa za kipato si tu kwa kampuni bali kwa wakazi wa kaunti ya Turkana iliyoko eneo hilo. Wanawake, wanaume na vijana wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kuchangamkia fursa ili kutekeleza miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan kwenye maeneo ya machimbo ya mafuta. Miongoni mwa walioitikia wito wa ni vijana wa Turkana ambao kupitia kikundi chao wananufaika bila hata kuajiriwa na kampuni ichimbayo mafuta ya Tullow.

Sauti
3'45"