Mtazamo wa jamii kuwa mwanamke kiongozi ametelekeza familia unasikitisha- Gavana Laboso
Mtazamo potofu wa jamii ya kwamba mwanamke anayejishughulisha na masuala ya uongozi hususan wa kisiasa hajali familia yake au hawezi kutunza familia hiyo ni wa kusikitisha Hiyo ni kauli ya Joyce Laboso, gavana wa kaunti ya Bomet nchini Kenya, akisema mtazamo huo na changamoto zingine zinaathiri ushiriki wa wanawake katika uongozi hususan siasa.