Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa jamii kuwa mwanamke kiongozi ametelekeza familia unasikitisha- Gavana Laboso

Mtazamo wa jamii kuwa mwanamke kiongozi ametelekeza familia unasikitisha- Gavana Laboso

Pakua

Mtazamo potofu wa jamii ya kwamba mwanamke anayejishughulisha na masuala ya uongozi hususan wa kisiasa hajali familia yake au hawezi kutunza familia  hiyo ni wa kusikitisha Hiyo ni kauli ya Joyce Laboso, gavana wa kaunti ya Bomet nchini Kenya, akisema mtazamo huo na changamoto zingine zinaathiri ushiriki wa wanawake katika uongozi hususan siasa.

Bi. Laboso amesema fikra kama hizo potofu ndio zinazidi kuongeza pengo la uwakilishaji wa kundi hilo kwenye bunge au vyombo vingine. Bi Labobo ambaye ni mmoja wa magavana watatu wanawake kati ya magavana 47 nchini Kenya alitoa mtazamo huo wakati wa mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa ya kiswhaili ya Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hivi karibuni.

Kwanza kabisa anafafanua  mtazamo hasi wa wanawake viongozi.

Audio Credit
Patrick/ Grace
Audio Duration
3'57"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman