Hadithi simulizi zaimarisha elimu kwa kuleta ladha tofauti
Msemo wa mwacha mila ni mtumwa umedhihirika kufuatia mradi unaotekelezwa katika shule moja mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako ajuza wanaopatiwa msaada katika kituo cha malezi ya wazee shuleni hapo wameajiriwa kusimulia hadithi kwa wanafunzi ambazo zinatoa elimu na mafunzo kuhusu masuala mbalimbali.
Mpango huo unarejea utamaduni wa kiafrika wa siku za nyuma ambapo mababu zetu walipitisha ujumbe au kutoa mafunzo kwa jamii kwa njia ya hadithi walizosimulia.