Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi za hadithi zarejeshwa kwa watoto mkoani Morogoro nchini Tanzania

Simulizi za hadithi zarejeshwa kwa watoto mkoani Morogoro nchini Tanzania

Pakua

Katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa Tanzania, shirika moja la kiraia limebuni mbinu za kuleta pamoja wazee na watoto kama njia mojawapo ya kuimarisha utamaduni na kuboresha stadi za maisha kwa watoto na vijana.

 Shirika hilo Childhood Development Organisation, CDO, limeanzisha mbinu huyo ambayo kwao wazee wanasimulia hadithi kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja.

Fasihi hii simulizi inaonekana kuwa ilianza kupotea lakini shirika hili linaunga mkono harakati za  Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO za kutumia mbinu za kiasili kufundisha vijana.

John Kabambala wa radio washirika Tanzaniakidstime FM kutoka Morogoro ametembelea ofisi za shirika hilo zilizoko Mzumbe na kukuta simulizi zikiendelea.

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kabambala
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
PICHA: Tanzaniakidstime/John Kabambala