Ni wakati wa vijana kuamka na kupiga kelele
Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la kazi duniani, ILO inaonyesha kuwa soko la ajira kwa vijana katika nchi zinazoendelea hususan katika bara la Afrika, Amerika kusini na Asia kusini linazidi kusuasua kutokana na ukuaji mdogo wa uchumi katika nchi hizo.
Umoja wa mataifa katika ajenda 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs , inazihimiza serikali, mashirika na asasi za kiraia kuwekeza katika taaluma au miradi itakayowawezesha vijana kujikwamuwa na tatizo la ajira ifikapo mwaka2030.