Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania tumepiga hatua kumjumuisha mwanamke katika huduma za kifedha: Nangi Massawe

Nangi Moses Massawe  kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha akizungumza na Flora Nducha wakati akiwa ziarani jijini New York Marekani.
UN News
Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha akizungumza na Flora Nducha wakati akiwa ziarani jijini New York Marekani.

Tanzania tumepiga hatua kumjumuisha mwanamke katika huduma za kifedha: Nangi Massawe

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo.

Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. 

Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha. 

Nagi aliyekuwa hivi karibuni hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW68 amesema Tanzania inaendelea na juhudi za kuhakikisha lengo hilo linatimia “Mchakati Tanzania alianza mwaka 2006 lakini ilipofika mwaka 2017 ndio tulianza kutathimini kwa kina nani aliyeachwa nyuma na tukabaini kwamba wanawake walikuwa wameachwa nyuma wengi kutokana na masuala ya mila na desturi, kutokuwa na elimu ya kutosha , kutoweza kumiliki mali kama ardhi ambazo mara nyingi zilitumika kama dhamana ya kupata mikopo na pia kukosa vitambulizo hali iliyochangia wanawake kuwa wachache wanaoweza kujumuishwa katika huduma hizo kuliko wanaumme.”

Anasema wanawake walikuwa ni asilimia 60 pekee waliweza kupata huduma hizo ikilinganishwa na asilimia 71 ya wanaume.

Nangi Moses Massawe  kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha akizungumza na Flora Nducha wakati akiwa ziarani jijini New York Marekani.
UN News
Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha akizungumza na Flora Nducha wakati akiwa ziarani jijini New York Marekani.

Baada ya kubaini sababu nini kinafanyika kuwajumuisha?

Bi. Nangi amesema mikakati ya makusudi ikiwekwa na serikali kuhakikisha mwana mke anajumuishwa haraka na ipasavyo katika huduma hizo za kifedha .

“Kwanza tulijitahidi haraka sana kuhakikisha wanawake wanaweza kupata vitambulisho na hilo tulilifanikisha, lingine ni kuhakikisha wanawake waweze kumiliki ardhi ili ziwasaidie katika kuweza kupata mikopo na hilo lilifanikishwa na vilevile tuliandaa mkakati maalum kwa upande wa elimu ambapo elimu ya masuala ya kifedha ilijumuishwa katika mitaala ya shule kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu ili wakue wakitambua umuhimu wa kujumuishwa katika masuala ya kifedha na elimu hiyo inajumuisha wote wasichana na wavulana.”

Ameendelesa kusema kuwa baada ya hatua hizo kuanza kutekelezwa mwaka 2023 tathimini nyingine iliyofanyika imeonyesha pengu kupungua miongoni mwa wanaume na wanawake kwani sasa idadi ya wanawake wanaojumuishwa katika huduma hizo imeongezeka hadi asilimia 74 wakati wanaume ni asilimia 77.

Njia gani zinazotumika katika kumjumuisha mwanamke

Meneja huyo anasema wanawake katika jamii ya Tanzania wamegawanyika katika makundi mbalimbali kwani kuna wale wanaoishi mijini na wengine vijijini, kuna walio na elimu na wasio na elimu , kuna wanawake watu wazima na kuna vijana hivyo kwa kulingatia hilo wameanda mikakati kwendana na makundi hayo mathalani kwenye elimu ukiacha wale walio katika mfumo wa shule ambako elimu ya kifedha imejumuisha katika mtaala wanawafunza pia walio nje ya mfumo wa elimu.

Pia amesema “Tunaanggalia huduma ipi inamfaa nani nai pi haimfai, mfano tulianzisha huduma inaitwa Timiza ambayo iliangalia wanawake wengi wajasiriamali mfano kina mama lishe ambapo wakijisajili wanaweza kukopa fecha asubuhi kuendesha shughuli zao na kisha kuzirejesha jioni.”

Ameongeza kuwa kutokana na mahitaji sasa wanawapa wataalam mbalimbali fursa ambao wako tayari kuandaa hizo huduma na Benki Kuu inawatengenezea mazingira ya kufanya majaribio na kisha kuingiza huduma hiyo sokoni kwa wananchi.

Wanawake wakisuka wakati wakisikiliza redio katika kijiji kimoja kwenye Kisiwa cha Tumbatu, Tanzania.
UNESCO/Leandro Pereira-França
Wanawake wakisuka wakati wakisikiliza redio katika kijiji kimoja kwenye Kisiwa cha Tumbatu, Tanzania.

Je huduma hizo zinamfikia kila mwanamke kwa usawa?

Bi. Nangi amesema hilo pia ni suala lililotupiwa jicho kwa kina hasa kutokana na utofauti wa mazingira wanamoishi wanawake hao.

Kuhusu changamoto ya wanawake kuwa na dhamana ya kupata mikopo amesema hilo waliliona na ndio maana kwa sasa hata “Kundi ni dhamana, lakini kwa makundi mengine ya wanawake ambao hawana ardhi, sasa hivi kama nchi tunadaa sheria ambayo itaruhusu hata zile bidhaa ambazo zinahamishika kama magari ziweze kutumika kama dhamana.”

Ameendelea kusema kuwa katika mchakato huo mzima changamoto kubwa ni ufikiaji hivyo “Kitu cha kwanza tunachokiangalia ni kufikiwa wale walioko mjini tunasema karibu asilimia 100 wamefikiwa lakini wale walioko vijijini ni asilimia 86 tu ndio waliofikiwa na huduma hizo hivyo kuna asilimia ya wanawake ambao bado hawajafikiwa.”

Hata hivyo amesema kitu kikubwa ni kubaini ni wapi waliko ili waweze kufikiwa na sehemu kubwa ya kitu kinachoweza kufanikisha hilo ni teknolojia.

Bi. Nangi ametoa wito kwa wanawake wote nchini Tanzania “Kuwa tayari kupokea huduma hizo kwani utayari ni muhimu sana kupokea hili suala linapokuja mbele yao, tusipokuwa tayari hatutoweza kufanya chochocte.”