Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuongeza mlo shuleni Afrika ni muhimu kwa mustakbali wa bara hilo: WFP

Mradi wa ‘mifumo jumuishi ya chakula’ nchini Namibia unaangazia lishe bora na mbinu bora za ukulima katika masshule kama sehemu ya mpango wa kulisha watoto shuleni unaoungwa mkono na WFP.
© WFP/Claudia Altorio
Mradi wa ‘mifumo jumuishi ya chakula’ nchini Namibia unaangazia lishe bora na mbinu bora za ukulima katika masshule kama sehemu ya mpango wa kulisha watoto shuleni unaoungwa mkono na WFP.

Kuongeza mlo shuleni Afrika ni muhimu kwa mustakbali wa bara hilo: WFP

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ikiwa leo ni siku ya mlo shuleni barani Afrika, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema pamoja na hatua kubwa zilizopigwa katika mchakato huo ni muhimu kutambua kwamba wanafunzi wengi lazima wapewe hakikisha la mlo endelevu shuleni.

Harufu kali ya maharagwe yanayochemka na ugali wa unga wa mahindi unaoungua iliyotamalaki Kwenye shoroba za shule ni moja ya vitu ninayoweza kukumbuka kutoka siku zangu nikikua katika shule ya bweni ya serikali huko Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania.

Wakati mwingine, harufu hiyo ilibadilika na kuwa ya kabichi inayochemka na wali unaoungua. Hili lilikuwa jambo la pekee kwetu, na ilitubidi kuhakikisha kwamba tulipanga foleni kwenye bwalo la kulia chakula kwa wakati wanakumbuka wanafunzi hawa.

Wanafunzi wawili katika shamba la mahindi iliyopandwa ili kuhakikisha lishe bora shuleni katika eneo la Karamoja nchini Uganda.
© WFP/Joel Ekström
Wanafunzi wawili katika shamba la mahindi iliyopandwa ili kuhakikisha lishe bora shuleni katika eneo la Karamoja nchini Uganda.

Hicho kilikuwa chakula changu cha mchana na chakula cha jioni kwa miaka kadhaa: kisicho na Ladha wala viungo vya kupendeza, siku baada ya siku, bila mapumziko.

Baada ya muda, sote tulijifunza ‘kufurahia’ milo yetu. Tuliweza kuongeza vionjo vyovyote, au vitu vilivyopigwa marufuku kama vile pilipili, ketchup, majarini au kachumbari (ambayo niliipenda sana) ya embe wakati wowote tulipoweza kuviingiza ndani ya shule.

Huu ukawa mwanzo wa mahusiano yangu ya chuki na maharagwe na ugali. Kwa miaka iliyofuata sikuweza kuvuta harufu ya maharagwe yanayochemka.

Ilichukua miaka mingi kurejesha amani na chakula hiki ambacho ni kikuu katika sehemu kubwa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Msichana katika shule moja huko Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akifurahia maharagwe katika sahani yake ya kwa chakula cha mchana.
© WFP/Vincent Tremeau
Msichana katika shule moja huko Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akifurahia maharagwe katika sahani yake ya kwa chakula cha mchana.

Milo shuleni tangu wakati huo imeongezeka na kubadilika, kutokana na ushirikiano wa karibu kati ya watunga sera, wataalam, na mashirika kama vile WFP, ili kutetea dhamira thabiti za kisiasa na kuunga mkono serikali za kitaifa katika kuandaa na kutekeleza sera na mifumo ya udhibiti inayozingatia masuala yote mawili ambayo ni ubora wa chakula na kiwango katika kuanzisha milo shuleni.

Leo, milo mbalimbali yenye afya bora iko kwenye menyu za shule, ikiwa ni pamoja na bidhaa kama vile nafaka, jamii ya viazi na mizizi, jamii ya kunde, mboga mboga na matunda, pamoja na nyama na maziwa uchaguzi ambao unategemea uwezo na upatikanaji wake.

WFP imekuwa mstari wa mbele katika mabadiliko haya, ikiendesha ajenda ya lishe darasani ili kuhakikisha kila mtoto anapata milo yenye afya na lishe shuleni.

Mlo shuleni ni lengo kuu la WFP katika Jamhuri ya Congo ambapo tunafikia wanafunzi zaidi ya 173,000 katika shule za msingi 532, kama hii katika idara ya Plateaux.
© WFP/Gabriela Vivacqua
Mlo shuleni ni lengo kuu la WFP katika Jamhuri ya Congo ambapo tunafikia wanafunzi zaidi ya 173,000 katika shule za msingi 532, kama hii katika idara ya Plateaux.

Tangu mwaka 2022, nchi 48 kati ya 54 barani Afrika zimeweka sera za mlo shuleni. Hii ni hatua muhimu, kwani sera husaidia kuimarisha ahadi za kitaifa, kufafanua malengo na mikakati, na kuweka miongozo na viwango vya lishe kwa ajili ya programu za kulisha wanafunzi shuleni.

Programu za kulisha watoto shuleni kupitia chakula kinachozalishwa nyumbani (HGSF) ambazo hutoa chakula salama, tofauti na chenye lishe bora, kinachopatikana kutoka kwa wakulima wadogo na bustani za shule hutoa motisha kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni. Pia husaidia kujenga uwezo na kusaidia maisha ya wakulima wadogo na jamii za wenyeji.

Uchunguzi unaonyesha kuwa milo shuleni sio tu inapunguza njaa na kuboresha afya na lishe, lakini pia huongeza tija ya nchi na kuruhusu watoto kuelewa vyema uhusiano kati ya kile tunachokuza na kile tunachokula.

Watoto wanafurahia chakula cha mchana katika shule moja ya kambi ya wakimbizi katika eneo la wasomali nchini Ethiopia.
© WFP/Michael Tewelde
Watoto wanafurahia chakula cha mchana katika shule moja ya kambi ya wakimbizi katika eneo la wasomali nchini Ethiopia.

Hata hivyo, licha ya maendeleo yote yaliyofanywa kwa miaka mingi, si kila mtoto ana bahati ya kupata mlo mzuri shuleni. Programu nyingi za kulisha shuleni bado zinakabiliana na ufadhili duni na usiotabirika.

Kulingana na WFP, programu za mlo shuleni barani Afrika zinasaidia asilimia 55 ya wanafunzi katika nchi za kipato cha kati, asilimia 15 tu ya watoto katika nchi zenye kipato cha chini wanapata chakula shuleni.

Matokeo haya yanadhoofisha matarajio ya Bara la Afrika, yaliyoainishwa katika Ajenda ya Muungano wa Afrika ya mwaka 2063, ambayo ni pamoja na kuendeleza mtaji wa kibinadamu na kijamii wa Afrika (kupitia mapinduzi ya elimu na ujuzi) na kuwa na raia wenye afya na lishe bora.

Ili kufikia hili, kuongeza milo ya shule lazima iwe kipaumbele.

Shughuli kuu ya WFP katika Jamhuri ya Congo ni kulisha watoto shuleni, na inatekelezwa katika shule za msingi za umma 532, na kufikia zaidi ya watoto wa shule 171,000.
© WFP/Gabriela Vivacqua
Shughuli kuu ya WFP katika Jamhuri ya Congo ni kulisha watoto shuleni, na inatekelezwa katika shule za msingi za umma 532, na kufikia zaidi ya watoto wa shule 171,000.

Serikali za Afrika na washirika wao wa maendeleo lazima waendelee kuwekeza katika mlo shuleni, ili kuhakikisha watoto wote wanaweza kupata mlo wenye afya, bila kujali wapi wanakulia.

Siku ya mlo shuleni Afrika ni fursa nzuri ya kutafakari na kuweka mikakati ya njia bora ya kuboresha na kuongeza programu za ulishaji mashuleni.

Hili ni muhimu kwa afya na ustawi wa Bara la Afrika na wananchi wake hasa kwa wale wanaotoka katika kaya zenye kipato cha chini katika jumuiya za vijijini, hili linaweza kuwa tumaini lao pekee la kupata mlo unaofaa kuwaruhusu kujifunza na kuwa raia wenye tija.

Watoto katika shule inayofadhiliwa na WFP katika eneo la Diffa nchini Niger.
© WFP/Abdoul Rafick Gaissa Chai
Watoto katika shule inayofadhiliwa na WFP katika eneo la Diffa nchini Niger.

Katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa chakula kama vile Sudan, Sudan Kusini, Somalia au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mlo shuleni inakuwa ndio njia ya maisha.

Habari njema ni kwamba ari ya kisiasa na kuunga mkono milo shuleni kunazidi kuchochewa na serikali chini ya uratibu wa Muungano wa Mlo Shuleni ambao ulianzishwa na serikali kuendesha hatua za kuboresha na kuongeza programu za chakula shuleni.

WFP ina zaidi ya miongo sita ya uzoefu wa kufanya kazi na serikali kusaidia na kufanikisha mipango endelevu ya mlo shuleni katika nchi zaidi ya 100 duniani kote.

Shughuli kuu ya WFP katika Jamhuri ya Congo ni kulisha watoto shuleni, inayotekelezwa katika shule za msingi za umma 532, na kufikia zaidi ya watoto wa shule 171,000.
© WFP/Gabriela Vivacqua
Shughuli kuu ya WFP katika Jamhuri ya Congo ni kulisha watoto shuleni, inayotekelezwa katika shule za msingi za umma 532, na kufikia zaidi ya watoto wa shule 171,000.

Mwaka 2022, kupitia msaada wa WFP kwa serikali kuanzisha au kupanua wigo wa programu za kitaifa za mlo shuleni, tulisaidia kwa njia isiyo ya moja kwa moja maisha ya watoto milioni 107. 

WFP pia ilitoa chakula chenye afya, vitafunwa, au kuhamisha fedha taslimu kwa zaidi ya watoto milioni 20 wa shule mwaka huo, ambapo karibu nusu yao wako Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Juhudi hizi zote na uzoefu wa kimataifa zimekuwa zikiunda programu za chakula shuleni ili kwamba, leo, wanafunzi wadogo barani Afrika wana uzoefu mzuri zaidi wa milo shuleni kwa hivyo ni muhimu kwamba waendelee kukipata chakula hicho.

Kwa upande wangu, kila siku ninaendelea kujifunza zaidi kuhusu thamani ya lishe ya maharagwe, na kwa nini walitufanya tuendelee kula miaka hiyo yote. Mbali na hilo, harufu sio mbaya kabisa!