Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamwe hatutowasahau wahanga wa mauaji ya maangamizi makubwa ya Holocaust: Guterres

Kambi ya maangamizi ya Auschwitz-Birkenau kusini mwa Poland
Unsplash/Jean Carlo Emer
Kambi ya maangamizi ya Auschwitz-Birkenau kusini mwa Poland

Kamwe hatutowasahau wahanga wa mauaji ya maangamizi makubwa ya Holocaust: Guterres

Haki za binadamu

Katika siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya maangamizi makubwa ya Holocaust Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kupitia ujumbe maalum wa siku hii amesema " leo  tunawaomboleza watoto milioni 6 wa Kiyahudi, wanawake, na wanaume waliouawa katika mikono ya Manazi na washirika wao, na tunawaenzi Waroma na Wasinti, watu wenye ulemavu, na wengine wengi sana ambao waliteswa na kuuawa katika Maangamizi Makubwa ya Holocaust. 

Ameongeza kuwa “Tunaheshimu kumbukumbu zao. Tunasimama pamoja na walionusurika, familia zao, na vizazi vyao. Tunaahidi kutowasahau asilani, wala kuwaacha wengine wasahau ukweli wa kile kilichotokea. Na tunatambua jinamizi la kutishalinaloletwa na siku hii ya ukumbusho katika nyakati zetu.

Guterres ameweka bayana kuwa, "chuki dhidi ya Wayahudi iliyochochea mauaji ya Holocaust haikuanza na Manazi, wala haikuishia kwa kushindwa kwao kwani leo, tunashuhudia chuki ikienea kwa kasi ya kutisha.  Mtandaoni, imehama kutoka pembezoni hadi kwenye kitovu cha majukwaa.”

Afisa wa polisi wa Kijerumani akikagua karatasi za utambulisho za Wayahudi katika makazi ya Krakow ghetto. Poland. Circa 1941.
© National Archives in Krakow
Afisa wa polisi wa Kijerumani akikagua karatasi za utambulisho za Wayahudi katika makazi ya Krakow ghetto. Poland. Circa 1941.

Kutokumbatia utofauti ni hatari kubwa

Katibu Mkuu amesistiza kuwa leo na kila siku ni lazima kukumbuka kwamba  “Unyanyasaji na kudharau utofauti ni hatari kwa kila mtu. Kwamba hakuna jamii iliyo na kinga dhidi ya kutovumiliana na mengine mabaya zaidi. Na chuki dhidi ya kundi moja ni chuki dhidi ya wote.”

 Zaidi ya hayo, Guterres amesema aanakumbuka alichosema Rabi Mkuu wa zamani wa Uingereza, Jonathan Sacks, ambaye alisemakwamba ikumbukwe kuwa "Chuki inayoanzia kwa Wayahudi haiishii kwa Wayahudi. Na kwa hivyo leo, hasa kutokana na mashambulizi ya kigaidi ya Oktoba 7 yaliyofanywa na Hamas, lazima tuazimie kusimama dhidi ya nguvu za chuki na migawanyiko."

Amehitimisha ujumbe wake kwamba, kusema kwamba "Lazima tushutumu, bila shaka, wakati wowote na popote tunapokumbana na chuki, kama vile tunavyopaswa kulaani aina zote za ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kidini, ikiwa ni pamoja na chuki dhidi ya Waislamu na unyanyasaji wa jamii za Wakristo walio wachache” 

Amesisitiza kuwa “Tusinyamaze kamwe mbele ya ubaguzi, na kamwe tusivumilie kutovumiliana. Tuzungumzie haki za binadamu na utu wa wote. Tusisahau kamwe ubinadamu wa kila mmoja wetu, na tusifumbe macho kwa wote wanaokabiliana na ubaguzi na mateso, hebu tuseme waziwazi hauko peke yako, Umoja wa Mataifa uko pamoja nawe.”