Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita, mabadiliko ya tabianchi na AI ni changamoto tunazopaswa kuzishughulikia haraka: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia jukwaa la 2024 la uchumi duniani mjini Davos Uswis.
United Nations/Stephanie Tremblay
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia jukwaa la 2024 la uchumi duniani mjini Davos Uswis.

Vita, mabadiliko ya tabianchi na AI ni changamoto tunazopaswa kuzishughulikia haraka: Guterres

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis akigusia changamoto mbalimbali zinazpoikabili dunia hivi sasa kuanzia vita inayoendelea Gaza na kwingineko, hali ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya akili mnemba au AI.

Kuhusu mizozo hotuba hiyo imegusa kwa kirefu hofu ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa na majanga ya kibinadamu hususan katika mizozo inayoendelea kama vile Gaza na Ukraine akisema kuanzia uvamizi wa Urusi Ukraine hadi Sudan na hivi karibuni kabisa Gaza, pande husika katika mizozo hiyo zinapuuza sheria za kimataifa, zinakiuka mikataba ya Geneva na hata kukiuka katiba ya Umoja wa Mataifa.

Mathalani kuhusu Gaza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema “Mzozo usioisha huko Gaza tayari umesababisha ukosefu wa usalama wa kikanda na ni ushahidi wa wazi kwamba jumuiya ya kimataifa inahitaji kuweka uzito wake kwenye suluhisho la Mataifa mawili katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ili kutatua mgogoro uliodumu muda mrefu mara moja na kwa wote".

Suluhu ya mataifa mawili Israel- Palestina

Akizungumza katika Kongamano hilo la Kiuchumi la Dunia la kila mwaka huko mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya kinyama yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 Oktoba ambapo takriban watu 1,200 waliuawa kwa kuchinjwa kusini mwa Israel na wengine 250 kuchukuliwa mateka.

Na huku kukiwa na ripoti za mashambulizi makubwa yanayoendelea ya Israel ambayo yamesababisha makumi ya maelfu ya raia kuuawa na kusababisha maonyo ya mara kwa mara kutoka kwa wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu njaa na magonjwa yanayowanyemelea watu milioni 1.9 waliokimbia makazi, Bwana Guterres amesema  hofu ya kusambaa kwa mzozo huo tayari imeaanza inafanyika.

Ameonya kwamba “Dunia imesismama ikiangangalia raia hususani wanawake na watoto wakiuawa, kulemazwa, kushambuliwa kwa mabonmu, kufurushwa makwao na kunyimwa haki ya misaada ya kibinadamu.”

Na amerejea wito wa usitishwaji mapigano mara moja na kuwa na mchakato ambao utaelekea kuleta amani ya kudmu kwa Israel na Palestina kwa misingi ya kuwa na mataifa mawili akisistiza kwamba “Hii ndio njia pekee ya kukata shina la madhila na kuzuia mzozo huo kusambaa hali ambayo itawasha moto katika ukanda mzima.

Wapalestina wakikimbia kutoka Kaskazini mwa Gaza na kwenda eneo la kati na kusini mwa Gaza.
© UNRWA/Ashraf Amra
Wapalestina wakikimbia kutoka Kaskazini mwa Gaza na kwenda eneo la kati na kusini mwa Gaza.

Migogoro tayari inaongezeka

Katibu Mkuu amesema makabiliano makali kabisa kati ya Israel na Lebanon ambapo mabadilishano ya maroketi na silaha kwenye mpaka na Israel tayari yamegharimu maisha ya watu na hii itakuwa maafa makubwa.

Ameongeza kuwa ongezeko lolote la machafuko "linahitaji kuepukwa kwa gharama yoyote," kama vile mashambulizi ya wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwenye meli katika Bahari ya Sham yameonyesha kuwa juhudi zote za kutatua mgogoro wa Gaza hazikutosha.

Ameendelea kusema kwamba "Ni muhimu sana kushughulikia hali ya kibinadamu huko Gaza, ni muhimu sana kuwa na usitishaji wa mapigano wa kibinadamu, lakini tunahitaji kutafuta mara moja na kwa wote ahadi kamili ya jumuiya ya kimataifa kwa ufumbuzi wa Mataifa mawili kuwepo la Israeli na Palestina kama msingi wa Mashariki ya Kati tulivu na yenye amani kwa manufaa ya kila mtu.”

Wapalestina waliotawanywa wakiishi katika shule inayo
© UNRWA/Ashraf Amra
Wapalestina waliotawanywa wakiishi katika shule inayo

Dunia inaendelea kuchemka na joto

Pia katika hotuba yake Bwana Guterres ameelezea wasiwasi kuhusu changamoto ya tabianchi na ongezeko la joto duniani akisema nchi zimekumbwa na tabia ya kutochukua hatua na ubinafsi katia masuala ya maendeleo na matumizi ya mafuta kisikuku yameifanya dunia kushindwa kushikamana kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuchochea ongezeko la joto duniani “ Nchi zinaendelea kuzalisha hewa chafuzi, sayari yetu inazidi kuchemka kuelekea nyuzi joto 3celisius, ukame, vimbunga, moto wa nyika na mafuriko winaathiri nchi na jamii.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema "Sekta ya mafuta imezindua kampeni nyingine ya mamilioni ya dola ili kuendelea kuathiri mabadiliko ya tabianchi kwa kuweka mafuta na gesi kutiririka kwa muda usiojulikana," 

Ameyasema hayo akisistiza jinsi mataifa mengi ambavyo yanaonekana "hayana uwezo wa kufanya kazi pamoja kukomesha tishio la mabadiliko ya tabianchi huku Uswisi  penyewe akisema “barafu inatoweka mbele ya macho yetu”.

Changamoto za kiuchumi

Kuhusu ukuaji wa kiuchumi Bwana Guterres amesema matatizo mengi ya dunia yanatokana na kutoshikamana kati ya "matajiri, wakubwa na wengine duniani", amewaambia hayo wasomi wa uchumi duniani, katika ombi la "mazungumzo mazito kati ya mataifa yaliyoendelea kiviwanda na mataifa yanayoibukia kiuchumi ambayo yamekuwa yakizama katika lindi la madeni".

Ameendelea kusema kwamba nchi za Kusini mwa ulimwengu zimelemewa na viwango vya juu vya riba kiasi kwamba zimeshindwa kuwadhibitishia raia wao kwamba utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) haijawahi kuwa muhimu zaidi kuliko sasa.

Ameongeza kuwa nchi nyingi  bado zinaendelea kuzalisha zaidi hewa chafuzi. 

Teknolojia ya kidijitali kama AI inabadili mifumo ya maisha
UN Photo/Elma Okic
Teknolojia ya kidijitali kama AI inabadili mifumo ya maisha

Furs ana athari za akili mnemba AI

Na kuhusu suala la Akili mnemba Katibu Mkuu amezungumzia hatari yake na uwezekano wa kuongeza pengo la usawa na tabia isiyofaa ya makampuni makubwa ya teknolojia "Teknolojia hii ina uwezo mkubwa wa maendeleo endelevu lakini kama Shirika la Fedha Duniani lilivyotuonya hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa wa kuzidisha ukosefu wa usawa duniani. Na baadhi ya makampuni yenye nguvu ya teknolojia tayari yanafuata faida kwa kutozingatia haki za binadamu, faragha kibinafsi na athari za kijamii,"

Amehitimisha hotuba yake kwa kwa kusisitiza hali muhimu na inayowezekana ya kujenga upya imani kwa ajili ya dunia iliyo salama na imara zaidi.