Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadili ya katiba ya UN yako katika tishio kubwa kuliko wakati mwingine wowote: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo, akitoa hotuba nchini Hispania baada ya kupokea tuzo ya Ulaya ya Carlos V.
© Juan Carlos Rojas
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo, akitoa hotuba nchini Hispania baada ya kupokea tuzo ya Ulaya ya Carlos V.

Maadili ya katiba ya UN yako katika tishio kubwa kuliko wakati mwingine wowote: Guterres

Amani na Usalama

Maadili ya utu na uhuru wa binadamu, yaliyoainishwa katika Mkataba wa kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945, hayajawahi kutishiwa hivyo, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo, akitoa hotuba nchini Hispania baada ya kupokea tuzo ya Ulaya ya Carlos V.

Katika kukabiliana na mashambulizi dhidi ya misingi ya Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema kuwa jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua tahadhari, na kuthibitisha tena maadili hayo."

Amani haipo na iliyopo ni dhaifu

Zaidi ya yote, "tunahitaji amani" Guterres amewaambia watazamaji waliokusanyika kwa ajili ya tuzo ya kifahari inayotetea ushirikiano wa kimataifa barani Ulaya, katika ukimbi wa kifalme wa Yuste, huko Extremadura, na kubainisha kuwa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya, ziliundwa kwa jina la amani baada ya janga la vita ya pili ya dunia.

Ameongeza kuwa "Amani inasalia kuwa nyota yetu ya Kaskazini na lengo letu la thamani zaidi. Bado mapambano ya amani yanaweza kuonekana wakati mwingine kama kazi ya kwaya. Leo tunaishi katika ulimwengu ambamo amani haipatikani na ni dhaifu.”

Amesema ghasia zimekithiri, katika sehemu nyingi sana za dunia, akitoa mfano wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ukiukaji wa wazi wa mkataba, wa Umoja wa Mataifa unaokuja baada ya kuyumba kwa uchumi kulikosababishwa na janga la coronavirus">COVID-19.

"Vita na machafuko ya kibinadamu yanaenea, wakati mwingine mbele ya macho yetu, lakini mara nyingi mbali na uangalizi. Ni vigumu zaidi, na vimeunganishwa, na athari zake zinaongezeka siku hadi siku.”

Amesema kuwa mlipuko wa ghasia wa ghafla kote nchini Sudan, ni kumbusho kwamba amani mara nyingi inaweza kusambaratika mara moja na haipaswi kamwe kudharauliwa au kuchukuliwa kirahisi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo, akitoa hotuba nchini Hispania baada ya kupokea tuzo ya Ulaya ya Carlos V.
© Juan Carlos Rojas
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo, akitoa hotuba nchini Hispania baada ya kupokea tuzo ya Ulaya ya Carlos V.

Kufanya kazi kwa ajili ya amani

"Lazima tufanye kazi ili kuleta amani na kuidumisha, kila siku, bila kuchoka",

Ameongeza kuwa” Katika ulimwengu ambao unajitenga, lazima tuzime migawanyiko, tuzuie kuongezeka na kusikiliza malalamiko."

Diplomasia lazima ichukue nafasi ya utawala wa kutumia bunduki, izingatie mazungumzo, upatanishi na usuluhishi.

Ili kufanya hivyo, wanawake wanapaswa kuchukua nafasi muhimu na kuwa na nafasi ya uongozi katika diplomasia.

Ameonyesha wasiwasi pia katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi  akisisitiza maoni yake kwamba uhai wa wanadamu sasa uko hatarini, endapo kasi ya mabadiliko ya tabianchi haiwezi kupunguzwa.

Amesema "Mabadiliko ya tabianchi yanasababisha moto, mafuriko, ukame, mfano hapa Hispania, na matukio mengine mabaya ya hali ya hewa katika kila bara. Kila mwaka matukio haya yanaondoa mamilioni ya watu ambao mara nyingi hulazimika kutafuta kimbilio katika nchi na jumuiya ambazo ziko hatarini kwa.”

Kadhalika, amesema kuchukua hatua kwa ajili ya sayari, pia ilikuwa ni hatua ya amani "Na kwa mantiki hiyo hiyo, kupunguza hewa chafuzi, kulinda mazingira yetu na kusaidia jamii zilizoathirika ni kuchukua hatua kwa ajili ya haki."