Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usuli wa mzozo Sudan: Ukosefu wa ushwari watishia Afrika nzima

Jengo la makazi ya watu kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum likiwa limeharibiwa baada ya kushambuliwa kwa kombora.
Mohammed Shamseddin
Jengo la makazi ya watu kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum likiwa limeharibiwa baada ya kushambuliwa kwa kombora.

Usuli wa mzozo Sudan: Ukosefu wa ushwari watishia Afrika nzima

Amani na Usalama

Misukosuko imetawala kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia nchini Sudan, tangu Rais wa zamani wa taifa hilo Omar Hassan El-Bashir apinduliwe mwezi Aprili mwaka 2019. Serikali ya mpito ya kiraia iliyowekwa madarakani baadaye mwaka huo, kupitia makubaliano ya kugawana madaraka kati ya viongozi wa kijeshi na wa kiraia, ilipinduliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi mwezi Oktoba mwaka 2021. Tangu wakati huo, taifa hilo halijawa na serikali inayoongozwa na raia.

Mchakato wa kisiasa uliofuata ukiratibiwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na Mamlaka ya maendeleo ya kiserikali, IGAD ulifanikisha kufikiwa kwa makubaliano yaliyotiwa saini mwezi Desemba mwaka 2022 kati ya jeshi na wadau muhimu wanasiasa wa kira, na hivyo kuchagiza juhudi za kurejesha serkali ya kiraia iliyochaguliwa kidemokrasia.

Na wakati huo huo, uchumi wa nchi unayumba, mapigano ya kikabila na vitendo vingine vya ghasia vimeongezeka, raia wakilipa gharama kubwa, watu wengi wamekufa, nyumba zimaharibiwa huko Darfur na majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Janga la kisiasa linaloendelea linachanganyika na kuendelea kwa malalamiko ya kisiasa na mzozano wa kugombea ardhi usiopatiwa suluhu  katika taifa hilo kubwa lenye watu milioni 48, taifa la tatu kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Maelfu ya wakimbizi wamevuka mpaka wa Sudan na kuingia Chad kutokana na mapigano yanayoendelea nchini mwao.
© UNHCR/Aristophane Ngargoune
Maelfu ya wakimbizi wamevuka mpaka wa Sudan na kuingia Chad kutokana na mapigano yanayoendelea nchini mwao.

Changamoto ngumu

Changamoto zinazokabili Sudan ni nyingi, miongoni mwao ni mahitaji ya kiutu na kiuchumi, kuhakikisha kuna usalama na haki, kuheshimu haki za binadamu, kujenga amani, kusongesha mpito wa kidemokrasia.

Ingawa hivyo, kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya mfumo wa kisiasa mwezi Desemba mwaka 2022, mchakato wa kisiasa uliendelea kusonga mbele mwanzoni mwaka huu huku juhudi zikielekezwa zaidi kwenye kutatua masuala yaliyosalia ili hatimaye kukamilisha nyaraka ya mwisho ya makubaliano ya kisiasa.

Mwezi Machi mwaka huu,Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, aliripoti kuwa wadau wa Sudan walikuwa wanakaribia kuliko wakati wowote ule kufikia suluhu ya kurejea kwenye utawala wa kiraia.

Kituo cha muda wa dharura cha UNHCR huko Renk nchini Sudan Kusini kinapokea watu waliokimbia makazi yao kutoka Sudan.
© UNHCR/Charlotte Hallqvist
Kituo cha muda wa dharura cha UNHCR huko Renk nchini Sudan Kusini kinapokea watu waliokimbia makazi yao kutoka Sudan.

Mapigano mapya yapeleka mrama mazungumzo ya kisiasa

Matumaini hayo ‘yaliota mbawa’ baada ya mapigano kuibuka tarehe 15 mwezi Aprili kati ya jeshi la serikali, (SAF), likiongozwa na Luteni Jenerali Abdel-Fattah Al-Burhan, na wanamgamob wa Rapid Support Forces (RSF), wakiongozwa na Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, wakiacha mamia ya watu wamekufa na maelfu kukimbia makwao.

Hata kabla ya kuanza kwa mapigano ya sasa, mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan tayari  yalikuwa yamefikia kiwango cha juu na kuvunja rekodi watu milioni 15.8 – takribani theluthi moja ya wananchi milioni 48 wa Sudan wanahitaij msaada wa kiutu mwaka huu pekee.

Ghasia za sasa zimesababisha kuweko kwa uhaba wa maji, chakula, dawa, mafuta ilhali bei za bidhaa muhimu ikiwemo usafiri zimeongezeka kupita kiasi.

Taifa hilo pia ni nyumbani kwa zaidi ya wakimbizi na wasaka hifadhi milioni moja, wakitokea Sudan Kusini, Eritrea, Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Yemen na Chad.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa pande kinzani kutishisha uhasama waa mara moj na kuruhusu raia waondoke kutoka maeneo yenye mapigano.

 

UN nchini Sudan

Umoja wa Mataifa umekuwa ukisaidia kipindi cha mpito wa kidemokrasia nchini Sudan kupitia juhudi zinazoongozwa na Ujumbe wake wa kusaidia mpito nchini Sudan, UNITAMS unaoongozwa na Mwakilishi Maalum Perthes.

Wakati mami ya watumishi wa Umoja wa Mataifa na familia zao wamehamishiwa kwa muda ndani na nje ya Sudan, Umoja wa Mataifa umeahidi kuendelea kufanya kazi yake muhimu ya kuokoa masiha kwa kutumia wafanyakazi wake walioko ndani nan je ya Sudan wakijikita kwenye vipaumbele vya sitisho endelevu la mapigano, kurejea kwa mazungumzo ya kisiasa na kupunguza machungu ya kiutu wanayokabiliana nayo wananchi wa Sudan.