Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto ya utotoni yatimizwa na sasa Anastacie ni shujaa wa chakula wa FAO

Anastacie Obama (kushoto) akifungasha kamba waliookwa kwa moshi tayari kwa kupeleka sokoni.
© T.Graphics
Anastacie Obama (kushoto) akifungasha kamba waliookwa kwa moshi tayari kwa kupeleka sokoni.

Ndoto ya utotoni yatimizwa na sasa Anastacie ni shujaa wa chakula wa FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Taifa la Cameroon linapatikana kwenye pwani ya bahari ya Atlantiki katika kona ambako Afrika ya Kati na Magharibi zinakutana. Wareno katika safari zao zama hizo waliita eneo hilo “Rio dos Camarões” au “Mto wa Kamba” kutokana na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha aina hiyo ya viumbe vya baharini.

 

Anastasie Obama kutoka Cameroon naye ametambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kuwa ni Shujaa wa Chakula wa shirika hilo wakati huu ambapo dunia inaadhimisha siku ya wanawake wa vijijini.Anastacie anasimulia safari yake katika mazungumzo yake na Umoja wa Mataifa.

Tangu utotoni, nilikuwa navutiwa sana kuona wanawake wakiandaa samaki na mazao mengine ya baharini. Nilipotimiza umri wa miaka 7 na bado naenda shuleni nilinunua Kamba kwa ajili ya shangazi yangu na niliwaoka kwa kutumia moshi na kisha kuuza. Hivi ndivyo ambavyo biashara yangu Yaoundé, mji mkuu wa Cameroon ndivyo ilianza miaka kadhaa iliyopita.”

Nilichanja kuni nyumbani na kuchoma Samaki hao aina ya Kamba na kusambaza kijijini. Ilikuwa ni kazi ndogo na hata sikuwa na jiko la kuoka. Mume wangu aliniunga sana mkono na nikaanza kupata wateja wengi na Kamba wakaanza kuuzwa nje ya nchi.

Kwa kuwa uwezo wetu wa vifaa ulikuwa mdogo, basi tulihaha hivyo hivyo na angalau kupata faida kidogo kulipia gharama za uendeshaji. Faida ilikuwa kidogo lakini tuliweza kuendelea.
Hii leo, Kamba ni zao linalooza Cameroon kwa kuuzwa nje ya nchi. Nimesikia kuwa sekta ya Kamba inaajiri takribani watu 1,500 na naamini kamba ni chakula chenye afya na lishe bora kinachoweza kuliwa na watu wengi.

Kamba sasa wanavuliwa kwa wingi Thailand  na hakuna milipuko ya magonjwa kutokana na teknolojia ya kisasa
© FAO/Rocco Rorandelli
Kamba sasa wanavuliwa kwa wingi Thailand na hakuna milipuko ya magonjwa kutokana na teknolojia ya kisasa

Ingawa hivyo janga la ugonjwa wa Corona au coronavirus">COVID-19 limesababisha kusinyaa kwa soko la ndani la kamba. Kama tungalikuwa na mtaji wa kutosha tungaliweza kuwa na majokofu ya kuhifadhi samaki wetu na kuwaoka kwa moshi tu pale ambapo kuna mteja anahitaji.

Mimi na wafanyabiashara wengine tumekuwa tunaungwa mkono na FISH4ACP, ambao ni mpango wa kimataifa wa kusaidia uvuvi endelevu na uendelezaji wa mazao ya baharí kwa nchi za Afrika, Karibea na Pasifiki.

Mradi huu unatusaidia kufungua zaidi soko la Kamba hapa Cameroon na kuongeza thamani ya mnyororo mzima wa zao hilo kuanzia baharini hadi mezani kwa mlaji na pia kufanya shughuli nzima kuwa endelevu.

Hatimaye kwa hatua hii tunaweza kuimarisha vipato vyetu na vile vile kuchangia katika ukuaji wa uchumi, uhakika wa upatikanaji chakula na kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na sekta hii ya uvuvi.