Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mama na bintiye wanapokea huduma katika Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza mnamo Aprili 2024.
© WHO

Gaza: Mkuu wa WHO atoa wito wa kukomeshwa hospitali kuzingirwa

Huku mashambulizi ya mabomu yanayofanywa na jeshi la Israel yakiendelea usiku kucha katika Ukanda wa Gaza, pamoja na uvamizi wa ardhini na mapigano makali, mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa tahadhari hii leo kwa wafanyakazi na wagonjwa katika hospitali iliyozingirwa ya Al-Awda iliyoko kaskazini mwa Gaza. 

Kipimo cha uchunguzi wa haraka wa VVU na kaswende ikitumiwa kwa mwanamke mjamzito nchini Kambodia.
© UNICEF/Antoine Raab

Muhtasari wa habari: Magonjwa ya Zinaa, Huduma za afya Gaza, Vita Kharkive Ukraine

Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini. Mathalani mwaka 2022, Nchi Wanachama wa WHO ziliweka lengo kubwa la kupunguza idadi ya kila mwaka ya maambukizi ya kaswende kwa watu wazima mara kumi ifikapo 2030, kutoka watu milioni 7.1 hadi milioni 0.71.