WMO: Pembe ya Afrika kushuhudia mvua juu ya kiwango mwezi Juni- Septemba
Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO limetangaza kuwa katika kipindi cha mwezi Juni mpaka Septemba nchi zilizoko katika pembe ya Afrika zinatabiriwa kuwa na mvua kubwa na hii ikijumuisha nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia ya kati na kaskazini, magharibi na pwani ya Kenya, sehemu kubwa ya Uganda, Sudan Kusini, pamoja na Sudan.