Mazingira ambayo mamlaka ya Israel inawashikilia Wagaza yanatia hofu kubwa: UN
Huku kukiwa na ripoti zaidi za mashambulio ya mabomu huko Gaza usiku wa kuamkia leo Jumanne, Umoja wa Mataifa na mashirika wadau wameelezea wasiwasi wao juu ya hali ya kikatili isiyo ya kibinadamu wanakoshikiliwa na mamlaka ya Israel washukiwa wa wapiganaji wa Kipalestina katika eneo la makazi “kukiwa na madai ya unyanyasaji dhidi yao kiasi kwamba wengine walilazimika kukatwa miguu kutokana na kufungwa pingu kwa muda mrefu”.