Jambo kubwa katika kusaidia wakimbizi ni mawasiliano- Rais Nyusi
Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akiwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani amezungumza na Idhaa ya Umoja na kufafanua kile ambacho wanafanya kusaidia wakimbizi wanaotokana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yaliyojihami kaskazini mwa nchi hiyo hususan mpakani mwa nchi yake na Tanzania tangu mwaka 2017.