Mradi wa Uganda Yield Fund wawasaidia wajasiriamali Uganda wakati wa COVID-19
Uganda Yield Fund ambao ni ufadhili kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD ikishirikiana na Muungano wa Ulaya, UE, na serikali ya Uganda, umeisaidia sekta binafsi nchini Uganda ambayo nayo imewezesha wajasiriamali wadogowadogo ili wasiathiriwe sana na hivyo kuwa na mnepo hata katika mazingira ya Covid-19.