Miji endelevu ni muhimu katika kurejesha maisha bora baada ya COVID-19
Miji itakuwa muhimu kwa ulimwengu kupata nafuu kutoka kwenye janga la COVID-19 na uchumi mbaya zaidi kwa miongo kadhaa, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa hii leo na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na makazi, UN-Habitat.