Zaidi ya wahudumu wa afya 10,000 barani Afrika wameambukizwa COVID-19: WHO
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO leo limeonya kuhusu tishio la janga la ugonjwa wa corona au COVID-19 kwa wahudumu wa afya barani Afrika.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO leo limeonya kuhusu tishio la janga la ugonjwa wa corona au COVID-19 kwa wahudumu wa afya barani Afrika.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa kuwapatia watu maskini zaidi duniani kipato cha kujikimu, TBI, kunaweza kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19.
Vurugu za mara kwa mara katika eneo la Jonglei na Pibor, mashariki mwa Sudan Kusini tayari zimewatawanya watu 60,000 na zinalemaza uhakika wa chakula na ustawi wa watu, mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la mpango wa chakula WFP na la chakula na kilimo FAO, yameonya kupitia taarifa iliyotolewa hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.
Nchini Yemen, vita vya wenyewe kwa wenyewe na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, vimeleta taabu kwa wananchi huku familia zikihaha kujinusuru na Umoja wa Mataifa ukiingilia kati kusaidia.
Mfuko wa Elimu Haiwezi Kusubiri, ECW umetoa dola milioni 19 ikiwa ni awamu ya pili kwa ajili ya kushughulikia hatua za dharura za elimu kwa wakimbizi na wenyeji wao katika nchi 10 wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Watoto zaidi ya 32 wamepoteza au kutenganishwa na mzazi mmoja au wote kutokana na Ebola tangu kuzuka kwa mlipuko mpya Juni Mosi kwenye jimbo la Equateur Magharibi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi.
Wataalam ambao ni wajumbe wa Baraza la ushauri kwa ajili ya masuala ya kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa (DESA) leo wamechapisha ripoti inayopendekeza mambo ya kuzingatia kwa ajili ya kujikwamua vyema baada ya janga la corona au COVID-19 duniani.
Mafunzo ya ujasiriliamali kwa vijana wakimbizi yanayotolewa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD kwa msaada wa serikali ya Norway na ushirikiano wa serikali ya Niger kwenye kambi ya wakimbizi ya Diffa nchini Niger, yameleta nuru kwa vijana wakimbizi akiweo Ya Kaou aliyekimbia vita vya Boko Haram nchini Nigeria.
Kutana na mkimbizi Hamidullah mwenye umri wa miaka 23. Baada ya kukimbia machafuko Afghanistan na kupokelewa na kukirimiwa na Kijiji cha Pessat-Villeneuve nchini Ufaransa kwa msaada wa shirika la Umoja wa sasa analipa fadhila kwa kuisaidia jamii inayomuhifadhi kupambana na janga la corona au COVID-19.